Nyaraka za URFIG – Uchangamuzi kuhusu :

OMC - Shirika la Biashara Ulimwenguni - WTO

 

 

Shirika la Biashara Ulimwenguni :

Mnamo mwezi mmoja kutakuwa na mkutano wa mawaziri

MILKI YA MASHARIKI YAJIDHIHIRISHA

 

Kamwe ulimwengu waukukuwa totauti kama ulivyo leo, mwanzoni mwa karne hili la 21. Kamwe shimo baina ya nchi tajiri na nchi maskini halikukuwa pana kama lilivyo leo. Kamwe upana baina ya Kaskazini na Kusini haukukuwa mkubwa kama ulivyo leo. Kamwe upinzani baina ya serikali za kaskazini na za kusini haukukuwa wazi siku kwa siku, katika mwezi huu wa mwisho mbele ya mkutano wa 4 wa mawaziri wa Shirika la Biashara Ulimwenguni unaotarajika mjini Doha, huko Katar.

Bila shaka, kwanza nchi tajiri zitapaswa kujibu juu ya hali hii ya hatari kwa binadamu. Kwa hiari nchi hizi zilipotosha nafasi nzuri iliyosababishwa na mwisho wa vita baridi pamoja na kugawanya ulimwengu katika makundi mawili ya kisera. Badala ya kuanzisha sera mpya ya kimataifa inayoheshimu sheria na kusaidiana baina ya watu, sera ya ushindi ya Marekani na Umoja wa Ulaya ilitawala. Katika filosofia hii twataja maafikiano ya Marrakech yaliyotiliwa sahihi mnamo mwaka wa 1994 baada ya duru ya Uruguay. Maafikiano haya hayana uhaki. Nchi maskini zalazimishwa kufanya mengi wakati nchi tajiri hazipazwi kufanya lolote lile. Maafikiano haya yanatumika bila haki katika Shirika la Biashara Ulimwenguni ambalo ni mtumwa wa nchi tajiri na makampuni yake ya kimataifa.

Tangu mkutano wa Seattle, nchi maskini, wiki baada ya wiki kuko mjini Geneva, zilipinga duru mpya ya mapatano ampayo ingelilipa nguvu zaidi Shirika la Biashara Ulimwenguni. Nchi masikini ambazo zi nyingi miongoni mwa nchi 142 ambazo ni wanachama wa Shirika hili zilihimiza kutimilika kwa makubaliano ya Marakech : utathmini wa mapatano kufuatana na mazingira mapya ya kijamii, ya kiuchumi na kitamaduni pamoja na kuandika upya maafikiano haya kufuatana na masharti mapya. Zikiongozwa na Muungano wa Ulaya pamoja na Marekani, nchi tajiri zilikata kata kata mapendekezo haya ya nchi maskini.

Tarehe 19 Septemba, mjini Geneva, upinzani huu umeonekana wazi. Marekani imeuonesha kinaganaga. Kwa upande wake, katika waraka nafiki, Muungano wa Ulaya umepinga marekebisho yoyote yale juu ya maafikiano yahusuyo haki za kitaaluma. Marekebisho haya yalikuwa yanatakika katika nchi maskini kwa ajili ya kupata madawa muhimu zaidi.. Nchi maskini zina lengo la kulinda faida nono ya makampuni ya madawa.

Nchi tajiri zaficha kushindwa kwa sera zake katika kundi la wengi duniani. Hali kadhalika, zinaendelea kifidhuli kutoa hotuba za kupiga vita umaskini. Muungano wa Ulaya umeanzisha kampeni kubwa ya kutetea duru mpya ya mapatano. Mapatano haya yangelihusu nyanja pana zaidi na zingelieneza uhuru wa biashara usio na mipaka. Sera hili zingeliotesha mizizi wale mwenye nguvu na kunyonga mwenye kukosa nguvu Uongozi wake wa Biashara ya dunia si halili : unaweka dunia yote mikononi mwa makampuni ya kaskazini.

Bali nchi hizi hazikuwa tayari kwa upinzani zinaokutana nao sasa : katika mkutano uliokuwa umeandaliwa mjini Geneva, mwishoni mwa mwezi wa Juni na mwishoni mwa mwezi wa Julai, ilidhihilika kwamba hakuna ukubaliano wowote ule kati ya nchi tajiri na nchi maskini juu ya nia ya duru mpya. Mwishoni mwa mwezi wa Julai, kuhusu nyanja 20 ambazo Muungano wa Ulaya unataka kuingiza katika duru mpya, hakukuwa na makubaliano licha ya nguvu za aina zote zilizotumiwa na Kamati ya Ulaya pamoja na serikali fulani ambazo zaficha kutokubaliana huku na kutoonyesha kwa wananchi wake sera zake za ukoloni mambo leo. Mwishoni mwa mwezi Julai, mataifa 49 ambayo ni maskini zaidi, katika mkutano wake huko Tanzania, zimeonyesha upinzani wake juu ya duru mpya. Tarehe 24 Septemba, mjini Abuja (Nigeria), licha ya mbinu zilizotumiwa hasa hasa na Kamati ya Ulaya kwa ajili ya kushawishi nchi maskini, mawaziri wa kiafrika , wote kwa pamoja, wamepinga upya duru hii.

Afrika yasema kwamba nchi za kiafrika hazitaki mapatano mapya ya kimataifa juu ya nyanja mpya ; hazina uwezo wa kutimiza masharti yatakayotokana na mapatano haya ; hazioni faida zitakayoitoa kwenye kuhurisha biashara ya nyanya mpya ; zina mashaka juu ya masharti zaidi, tena zinaogopa hatari ambayo ingesababishwa na kuongezeka kwa uwezo wa Shirika la Biashara Ulimwenguni ; hakuna makubaliano baina ya nchi wanachama wa Shirika la Biashara Ulimwenguni juu ya kuanzisha mapatano ya namna hii na makundi tofauti ya kikazi ndani ya Shirika la Biashara Ulimwenguni hayana budi kuendeleza zaidi uchunguzi katika uwanya huu.

Barani Asia, Inda imeeleza upya upinzani wake juu ya duru mpya. Katika mkutano wake wa tarehe 28 Septemba mjini Bangkok, mataifa 33 ya Asia na Pacifika yamelaumu ukosefu wa uangavu katika nyaraka zilizoandaliwa na Shirika la Biashara Ulimwenguni kwa ajili ya mkutano wa mawaziri ujao. Mataifa haya yalisema kwamba yangelipenda zaidi makubaliano mapya juu ya mapatano ya Marakech kuliko duru mpya.

Muungano wa Ulaya hauna la kusema juu ya upinzani huu. Marekani na nchi tajiri vile vile. Wanahabari wanawaunga mkono katika kuficha msimamo huu wa nchi maskini. Wananchi hudanganywa kwamba sera zake zakubalika katika nchi za kusini na kwamba upinzani unaosikika ni wa Wanaulaya na Waamerika wasio na dhamana ambao wanashughlikia maNGO’s.

Ni kweli kwamba tangu siku chache twasikia vyama fulani vyenye siasa za kijamii na kidemokrasia vikisema eti vinataka « utu zaidi katika utandalizi ».Vyama hivi vyaogofywa na mafanikio ya maandamano yanaopinga utandalizi. Walakini vyama hivi vinaendelea kuunga mkono Kamati ya Ulaya ambayo inafanya kazi kinyume na sera zinazoanza sasa kutetewa na vyama hivi. Utu huu ni kama ule wa watetezi wa ukoloni ule wa wenye kuviunga mkono vita vya kikoloni. Utu hauwezi kuwa ile imani ya kifidhuli iliojiita « kazi ya Ulaya ya kustaarabisha »

Tareha 26 Septemba, nchi tajiri zilipanda hatua zaidi. Ziliandika kwa kutumia mikono ya Shirika la Biashara Ulimwenguni nyaraka mbili zenye kudhaminika kwa nchi hizi kupitishwa katika mkutano ujao wa mawaziri. Waraka wa kwanza ni taarifa la kiwaziri ambalo lingelifungua rasmi duru mpya. Taarifa hili halizingatii mapendekezo ya nchi za kusini. Katika taarifa hili kumeandikwa mapendekezo yote ya nchi tajiri. Waraka wa pili unazingatia mbinu dhaifu dhaifu ambazo zingelitumia kwa kuchunguza njia za kutimiza maafikiano yaliopo.

Katika nchi maskini nyaraka hizi zilionekana kama matusi. Tarehe 2 oktoba, kwa niaba ya nchi 49 maskini zaidi, marozi wa Tanzania kwenye Shirika la Biashra Ulimwenguni alikumbusha kwamba nchi maskini haziwi tayari kwa duru mpya. Barozi alisema kwamba nchi hizi hazina uwezo wa kushiriki katika mapatano haya na kwamba zakosa uwezo wa kutimiza masharti ambayo yangelisababishwa na mapatano haya. Barozi wa Malaysia alitaka nchi tajiri ziache kushawishi kwa nguvu nchi maskini.

Bwana Pascal Lamy ambaye ni Kamishna wa Ulaya, bila shaka akihimizwa na hali ya ulimwengu leo, bila kutabasamu, tarehe 1 oktoba, alitangaza : « Duru mpya ingesaidia katika kupiga vita ugaidi ».

Unafiki wa nchi za Ulaya wakosa mipaka. Hotuba nzuri za kupiga vita umaskini zatolea na serikali zetu, wakati kwa upande mwingine serikali zizi hizi, kwenye pahali pa kutolewa uamuzi, huwa na misimamo ambayo huongeza zaidi umaskini na hali ya kutegemea nchi za kaskazini kwa nchi za kusini.

Bila kukawia, hatuna budi kukumbusha wajibu wake kila mbunge na kila waziri wetu. Kwani, hatimaye, sera za Muungano wa Ulaya na za Shirika la Biashara Ulimwenguni huamuliwa katika kila nchi mwanachama.

 

Dr Raoul Marc JENNAR

Mtafiti kwenye Oxfam Solidarité (Brussels) na kwenye URFIG (Paris)

9 oktoba 2001