Faharasa - Kronolojia

 

 

ASEAN : Muungano wa Nchi za Mashariki ya Asia ya Kusini (Association of South East Asian Nations) , ulianza mnamo mwaka wa 1967 ; makao yake makuu yanakuwa mjini Jakarta

CJEC : Mahakama ya Muungano wa Ulaya (Court of Justice of the European Comunities. Yalianza mnamo mwaka wa 1952. Mahakama haya yanahusu nchi zote za Muungano wa Ulaya. Makao yake yanakuwa nchini Luxembourg.

DSB: Ofisi ya Kusuluhu Mabishano (The Dispute Settlement Body). Inasimamia masilahi ya mabishano yanayozuka katika Shirika la Biashara Ulimwenguni

EBRD : Benki ya Ulaya ya Ukarabati na Maendeleo (European Bank for Reconstruction and Development). Ilianza mnamo mwaka wa 1991. Kazi yake ni kuendeleza mabadilishano kwenye uchumi wa soko la wazi katika nchi 27 za Ulaya wa Kati wa Mashariki na nchi huru za Jumuia ya Madola ya Uingereza. Ina makao yake mjini Landani.

ECB : Benki Kuu ya Ulaya (European Central Bank). Ilianza tareha 1 Juni, 1998. Inajumuisha Benki Kuu za nchi 11 na kuunda mfumo wa Euro. Ina makao yake huko Frankfurt-am-Main (Ujerumani).

EU: Muungano wa Ulaya, Mnamo mwaka wa 1991 jina hili lilipewa shirika la mataifa ya Ulaya lililoanzishwa mjini Roma katika mwaka wa 1957 na kuitwa baadaye Majimbo ya Ulaya.

FAO: Shirika la Chakula na Ulimaji Duniani (Food and Agricultural Organization). Lilianza mnamo mwaka wa 1945. Lina makao makuu yake mjini Roma

GATS: Maafikiano Makuu Kuhusu Biashara ya Huduma (General Agreement on Trade in Services), Yaliwa sahihi mjini Marrakech tarehe 15 Aprili 1994. Halmashauri ya Shirika la Biashara Ulimwenguni inayoshughlikia biashara ya huduma husimamia uendeshaji wa maafikiano haya

GATT: Maafikiano Makuu Kuhusu Ushuru na Biashara (General Agreement on Tariffs and Trade) (angalia kwenye Kronolojia)

GATT 1994: Maafikiano Makuu Kuhusu Ushuru na Biashara (General Agreement on Tariffs and Trade), yaliyoingizwa ndani ya makala yaliyoidhinishwa mnamo mwaka wa 1994, mwishoni mwa Duru ya Uruguay na kupewa jina la Maafikiano ya Marrakech.

IATA : Shirika la Kimataifa la Ubebaji kwa ndege (International Air Transport Association). Lilianzishwa mnamo mwaka wa 1945. Li mrithi wa Shirika la Kimataifa la Usafirishaji Angani (the International Air Traffic Association) lililonzishwa mjini Hague mnamo mwaka wa 1919. Ni shirika la kibiashara linaloshughulika na kazi ya makampani ya ndege duniani. IATA Lina wanachama 273 kutoka kwenye nchi zaidi ya 130. Makao makuu yake yanakuwa mjini Geneva.

ICFTU : Muungano wa Kimataifa wa Vyama vya Biashara Huria (International Confederation of Free Trade Unions). Ulianzishwa mnamo mwaka wa 1949. Kuna miongoni mwake mashirika 221 kutoka kwenye mataifa 148. Wanachama wote wake ni miliyoni 155. Una makao makuu yake mjini Brussels.

ICJ : Mahakama ya Kimataifa (International Court of Justice). Ni mahakama ya Shirika la Umoja wa Mataifa (UNO). Yanahukumu migogoro ya kisheria inayowasilishwa na mataifa. Uzinduzi wa Mahakama ulifanywa mwakani 1946. Ni mrithi wa Mahakama ya Kudumu ya Sheria ya Kimataifa (the Permanent Court of International Justice -PCIJ) yalioanzishwa mnamo mwaka wa 1922. Makao yake yanakuwa mjini Hague (Uholanzi).

ILO: Shirika la Kazi Duniani (International Labour Organization), lilianzishwa mnamo mwaka wa 1919; makao yake makuu yanakuwa mjini Geneva.

IMO : Shirika la Kiamataifa la Mambo ya Baharini (International Maritime Organization), lilianzishwa mnamo mwaka wa 1958; makao makuu yake yanakuwa mjini Landani.

IMF: Shirika la Kimataifa la Fedha (International Monetary Fund), lilianzishwa katika mwaka wa 1945; makao makuu yake yanakuwa mjini Washington.

LAS: Shirikisho la Mataifa ya Kiarabu (League of Arab States), lilianzishwa mnamo mwaka wa 1945; makao makuu yake yanakuwa mjini Kairo.

LDC : Nchi Masikini (Least Developed Countries). Nchi 49 – ambazo hazina wananchi zaidi ya miliyoni 75 – Wastani wa kipato cha kila mwananchi u chini ya dola za malekani 900. Tena, nchi hizi huorodheshwa kufuata upanuzi wa uchumi na maendeleo ya kijamii. Tangu mwaka wa 1971, Shirika la Umoja wa Mataifa lilipoanzisha rika hili, tarakimu ya nchi hizi imekuwa karibu maradufu.

MFA: Makubaliano yahusuyo Biashara ya Kimataifa ya vitambaa (Multifibre Arrangement concerning the international trade of textiles). Toleo lililobadilishwa la Makubaliano haya iliingiza neno nguo lenyewe katika Makubaliano ya Kimataifa ya Biashara ya Bidhaa (Multilateral Agreements on Trade in Goods) yaliyopitishwa mjini Marrakech mnamo mwaka wa 1994.

NAFTA : Makubaliano kuhusu Biashara Huria katika nchi za Marekani ya Kaskazini (North American Free Trade Agreement). Yalianza katika mwaka wa 1994. Yanahusu Canada, USA na Mexico.

OAS: Shirika la Madola ya Marekani (Organization of American States), lilianzishwa mnamo mwaka wa 1948; makao yake makuu yanakuwa mjini Washington.

OAU: Umoja wa Nchi Huru za Afrika (Organization of African Unity), ulianzishwa mnamo 1963; makao yake makuu yanakua mjiji Addis Ababa.

OIC: Shirika la Nchi za Kiislamu (Organization of the Islamic Conference), lilianzishwa mnamo 1969; makao makuu yake yanakuwa mjini Jeddah

OECD: Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na maendeleo (Organization for Economic Co-operation and Development), lilianzishwa mnamo wa 1960; makao yake makuu yanakuwa mjini Paris. Kano la Makubaliano ya Kimataifa kuhusu nyanja za Kitegauchumi (the Multilateral Agreement on Investment -MAI) mnamo mwaka wa 1998 yalikuwa kizuizi kikubwa kwa OECD (elementi fulani zake ziliingizwa katika mapatano ya ndani ya Shirika la Biashara Ulimwenguni).

OIF: Shirika la Kimataifa la Mataifa yatumiayo Lugha ya Kifaransa (Organisation Internationale de la Francophonie), lilianzishwa mnamo mwaka wa 1998; makao yake makuu yanakuwa mjini Paris.

TBT : Maafikiano kuhusu Vikwazo vya Kiufundi vya Biashara (Agreement on Technical Barriers to Trade). Mamoja kati ya maafikiano haya husimamiwa na Shirika la Biashara Ulimwenguni

TMB: Ofisi ya Uchunguzi wa Biashara ya Vitangaa (Textiles Monitoring Body), ilianzishwa na MFA: (Makubaliano yahusuyo Biashara ya Kimataifa ya Vitambaa (Multifibre Arrangement concerning the international trade of textiles)

TPRB: Ofisi Mpya ya Sera ya Biashara (The Trade Policy Review Body) inasimamia mbinu mpya za kufuata sheria za Shirika la Biashara Ulimwenguni zinazopaswa kuheshimiwa na nchi mwanachama kama inavyoujadiliwa.

TRIPS: Makubaliano yanayohusu haki za kazi za kitaaluma (Trade-related Aspects of Intellectual Property Rights Agreement), yalipigiwa sahihi mjini Marrakech kwenye tarehe 15 Aprili 1994. Halimashauri ya Shirika la Biashara Ulimwenguni inayohusu TRIPS inasimamia kutimizwa kwa Makubaliano.

UNO: Umoja wa Mataifa (United Nations Organization), ulianzishwa mnamo mwaka 1945; makao makuu yake yanakuwa mjini New York.

UNCTAC: Halmashauri ya Umoja wa Mataifa inayohusu Biashara na Maendeleo (United Nations Conference on Trade and Development), ilianzishwa mnamo mwaka wa 1964; makao makuu yake yanakuwa mjini Geneva.

UNEP: Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Taifa, ulianzishwa mnamo mwaka wa 1972; makao makuu yake yanakuwa mjini Nairobi.

UNESCO: Shirika la Umoja wa Mataifa Linaloshughlikia Elimu Sayansi na Utamaduni (United Nations Educational, Scientific and Cultural Organization), lilianzishwa mnamo mwaka wa 1945; makao makuu yake yanakuwa mjini Paris.

UNFCCC: Makubaliano ya Jumla ya Umoja wa Mataifa juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa (United Nations Framework Convention on Climate Change), yalianzishwa mnamo mwaka wa 1995; makao makuu yake yanakuwa mjini Bonn

UNFPA: Shirika la Umoja wa Mataifa Linaloshughlikia Jamii (United Nations Population Fund), lilianzishwa mnamo mwaka wa 1969; makao makuu yake mjini New York.

UNIDO: Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughlikia maendeleo ya Vianda (United Nations Industrial Development Organisation), lilianzishwa mnamo mwaka wa 1966; makao makuu yake yanakuwa mjini Vienna.

UNICEF: Shirika la Umoja wa Mataifa Linaloshughlikia Watoto (United Nations Children Fund), lilianzishwa mnamo mwaka wa 1946; makao makuu yake yanakuwa mjini New York.

WB: Benki ya Dunia (World Bank), ilianzishwa mnamo mwaka wa 1945 pale Bretton Woods. Jina la mwanzoni lilikuwa ni Benki ya Kimataifa inayoshughlikia Ukarabati na Maendeleo (International Bank for Reconstruction and Development); makao makuu yake yanakuwa mjini Washington.

WHO: Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughlikia Afya (World Health Organization), lilianzishwa tarehe 7 Aprili 1948. Terehe hii iliteuliwa kuwa siku kuu ya afya duniani. Mako makuu ya WHO yanakuwa mjini Geneva.

WIPO: Shirika la Kimataifa linaloshughlikia haki za Kitaaluma (World Intellectual Property Organization), lilianzishwa mnamo mwaka wa 1970; makao makuu yake yanakuwa mjini Geneva.

WTO: Shirika la Biashara Ulimwenguni (World Trade Organization), lilianzishwa na Maafikiano ya Marrakech yaliyopigiwa sahihi tarehe 15 Aprili 1994; makao makuu yake mjini Geneva.

 

Anwani za internet za mashirika haya zilitajwa katika marejeo

 

Kronolojia

 

1944: Kuanzishwa kwa Benki ya Dunia (WB) na kwa Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF). Nchi 50 zilishiliki kwenye mradi huu. Kulianzishwa tena Shirika la Biashara la Kimataifa (an International Trade Organisation -ITO), ambalo lingeliingizwa ndani ya mfumo wa Umoja wa Mataifa (UN) pamoja na mashirika mengine madogo madogo ya kiufundi ambayo yangeliundwa.

1946-1947: Kwa mwaliko Marekani ambayo inalipa msaada hafifu Shirika la Biashara la Kimataifa (ITO), nchi 23 zilikutania mjini Geneva na kujadili juu ya upunguzaji wa gharama za biashara; nchi hizi zilitia sahihi kwenye mapatano ya kwanza ya Maafikiano Makuu Kuhusu Ushuru na Biashara (GATT).

1948: Maafikiano Makuu Kuhusu Ushuru na Biashara (GATT) yalianza kazi rasmi; mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu biashara na kazi ulifanyika mjini Havana: mkataba wa Shirika la Biashara la Kimataifa (ITO) ukapitishwa.

1949: Pale Annecy, duru la pili la mapatano kati ya walioingia kwenye mkataba wa GATT. Nchi 13 zilishiriki.

1950: Serikali ya Marekani ilikataa kuidhinisha rasmi mkataba wa ITO.

1951: Pale Torquay, duru la tatu la mapatano ya GATT. Nchi 38 zilishiriki.

1956: Mjini Geneva, duru ya nne ya mapatano ya GATT. Nchi 26 zilishiriki.

1960-1961: Mjini Geneva, duru ya tano ya mapatano ya GATT. Nchi 26 zilishiriki.

1964-1967: Duru ya Kennedy, mapatano ya sita ya GATT. Nchi 62 zilishiriki.

1973-1979: Duru ya Tokyo, mapatano ya saba ya GATT. Nchi 102 zilishiriki.

1986: Duru ya Uruguay ilizinduliwa pale Punta del Este, mapatano ya nane ya GATT. Nchi 123 zilishiriki. Kwa mara ya kwanza, mapatano hayakuhusu peke yake ushuru wa forodha. Mapatano yalihusu pia kutokuwepo kwa vikwazo vya ushuru (sheria ya taifa) pamoja na maali asili, misaada ya fedha, vitegauchumi, huduma za binafsi na za umma, haki za kitaaluma, Biashara ya vitambaa, kilimo. Mbinu mpya za kusuluhu migogoro na uanzishaji wa shirika la kimataifa linalohusu usimamiaji wa maafikiano pia vilijadiliowa.

1994: Maafikiano ya Marrakech yalipigwa sahihi (kurasa 22,500).

1995: Maafikiano ya Marrakech yalitumika. Shirika la Biashara Ulimwenguni likaanzishwa.

1996: Mkutano wa kwanza wa mawaziri wa nchi za Shirika la Biashara Ulimwenguni mjini Singapore

1998: Mkutano wa pili wa mawaziri wa nchi za Shirika la Biashara Ulimwenguni mjini Geneva.

1999: Mkutano wa tatu wa mawaziri wa nchi za Shirika la Biashara Ulimwenguni uliitwa