URFIG – Habari za Afrika

 

Tarehe 25 mei, Jubilii 2000/Shirika linaloshughlikia madeni na maendeleo Afrika (CAD-Mali) pamoja na shirika la wanafunzi wa kiafrika huko nchini Mali (CONEAM), yamesherehekea siku kuu ya Afrika

 

            Alhamisi 24 mei 2001, kati ya saa tatu asubuhi na saa moja jioni, katika jumba Mémorial Modibo Keita, CAD-Mali na CONEAM yameandaa semina ya kuimarisha uwezo wa vijana barani Afrika.

            Semina hii ilikuwa na lengo la kufunza na kubadilishana mawazo. Wakufunzi 123 kutoka vyuo na vyuo vikuu tofauti vya Mali na wanayoyawakilisha mataifa 17 ya bara la Afrika, yaani Niger, Kameruni, Burkina Faso, Ivory Coast, Benin, Visiwa vya Komoro, Moritania, Kongo Brazzaville, Kongo Kinshasa, Togo, Djibuti, Afrika ya Kati, Gabon, Chadi, Guinea Konakri, Madagaska na Mali, waliyahudhuria mafunzo haya.

SHABAHA KUU LA SEMINA

            Kuhimiza na kuhamasisha wanafunzi wa kiafrika wanaoishi nchini Mali, ili waibuke makada wa kiafrika angalifu na wenye busara, walio tayari kutetea haki za kiuchumi jamiini.

SHABAHA DHAHIRI

            Kufunza viongozi wa makundi ya wanafunzi, watakaoendelea kazi ya kuhimiza na kuhamasisha wenzao ndani ya makundi watokamo.

AJENDA YA SIKU YA KUBADILISHANA MAWAZO

            Mada : Maendeleo ya Afrika – Madeni na Ujana

I. Asili ya kihistoria na ya kisasa ya mgogoro wa madeni

A . Ya kihistoria :

Urithi wa utumwa na ukoloni, mbinu za unyonyaji na udhibiti wa mataifa ya Afrika.

B. Asili za nje za kisasa :

-         Uharibifu wa hali ya mabadilishano ya kiuchumi

-         Migogoro ya mafuta (petroli)

-         Kushuka kwa kiwango cha riba na cha kubadilisha fedha za kigeni

C. Asili za ndani za kisasa :

-         Uongozi wa sekta ya umma, udhaifu wa kujiweza na ulaji rushwa

-         Ratiba mbovu za maendeleo ambazo hazizai matunda

II. Utatuaji wa migogoro

A.     Ratiba za marekebisho ya miundo (structural adjustement programs) :

-         Misingi ya kinadharia (mawazo ya uwanja huu)

-         Shabaha za ratiba za marekebisho ya miundo

-         Utathmini wa uhakiki

B.     Siasa ya kupunguza madeni

(Kufeli kwa siasa za marekebisho na za kuahirisha madeni)

-         Hatua za pande mbili

-         Hatua za pande mbili (hatua HIPC ya asili na ile iliyesahihishwa, CSLP)

-         Mtindo wa soko (ubadilishaji, ufitaji wa deni nk.)

III. Maendeleo ya Afrika, madeni na ulimwengushaji wa mambo ya dunia (Mondialisation)

A.     Mmomonyoko wa wajibu wa serikali na kuharibika kwa jamii (ukosefu wa kazi, umaskini, hali isiyo ya usalama nk.)

B.     Maendeleo yanayohimizwa na hali ya soko

C.     Shughli pevu za kuanzisha upya ukoloni (ubinafsishaji  wa mali ya umma, ulegezaji wa masharti, kutotiisha sheria nk.) na za kurudisha hali ya utumwa

IV. Ujana

-         Kuna mtazamo sahihi gani kwa ajili ya maendeleo ya vijana wa kiafrika

-         Ili maswali yote haya yaliyotajwa yawe na jibu, wanafunzi walisema nini ?

V. Hitimisho

            Kwa ajili ya mtindo mwingine wa maendeleo.

            Sherehe za kufungua na kufunga semina ziliongozwa na Bibi BARRY Aminata Toure, mwenyekiti, Bwana DAO Dounantie, katibu mkuu na Bwana Ibrahim Hamani Souley, katibu mtendaji wa CONEAM.

            Hotuba ya mwanzo ilisomwa na Bwana Sékou DIARRA, mkufunzi. Hotuba hii ilikuwa inahusu hasa hasa ajenda ya semina. Baada ya hotuba hii wanafunzi waliunda makundi manne. Kila kunda lilipewa mada ya kujadili.

            Vile vile, kila kundi (likiungwa mkono na mwanachama wa CAD-Mali) lilikuwa na wajibu wa kubadilishana mawazo na kufasiri mada ndogo moja kwa ajili ya kuielewa vizuri na kuibuni mitazamo sahihi.

            Baada ya kazi ya makundi, washiriki wote walikutania upya ndani ya chumba cha mkutano. Pale, kila kundi liliwasilisha uchangamuzi na mitazamo yake.

N.B : Katika siku za usoni tutawatumia ripoti ya kinagaubaga ya semina ya kufunza na kubadilishana mawazo, ili mtukosowe na mtupe mapendekezo yenu.

            CAD-Mali linataraji kuandaa mkutano wa mamna hii tarehe 09/06/2001. Katika shughli hii CAD-Mali litashirikiana na makundi na mashirika ya wanawake (CAFO).

 

Kwa niaba ya uongozi

Katibu Mkuu

 

Ofisi ya taifa ya CAD – Mali inayoshughlikia PPTE na umaskini nchini Mali

Bibi Barry Aminata Touré

Internet na E-mail ya bure Alta Vista http://www.altavista.fr

E-mail : samba@altavista.fr

 

Jubilé 2000/Coalition des Alternatives Africaines Dette et Développement (C.A.D-Mali) en collaboration avec la Conférence des Etudiants africains au Mali (CONEAM) ont commémoré le 25 mai, journée historique de l'Afrique