Tunayoyasadiki
Mwongozo wetu ni wa kimataifa. Kulimwengusha mambo ya dunia ni jambo linalotufurahisha, kwani hupunguza ubaguzi miongoni mwa binadamu. Hukaribisha pia mataifa na hurahisisha kuelea kwa umoja wa nchi za dunia, ambamo huzusha suala la kuanzisha, kwa kiwango cha dunia, mashirika yanayofanya kazi kiangavu na yanayochunguliwa. Ndiyo maana hatukubaliani na wale watangazaji wa habari wanawotumia neno la "wapinzani wa ulimwengushaji" bila kuchunguza kinaganaga msimamo wetu.
Bali hatukubali utandarizi (kufanya dunia iwe kijiji kimoja). Utandarizi huu ni namna ya kipekee inayotumiwa na wachumi wa biashara, wanasiasa na watangazaji wa habari kwa kuonyesha ulimwengu tuishimo kama tukio la kawaida lisiloweza kubadilika, kama upeo wa macho wa historia ya ulimwengu wenyewe.
Utandarizi ni chaguo, ni utashi wa watu fulani. Twatupilia mbali chaguo hili, twapinga na twakana kanakana utashi huu, kwani shabaha la utandarizi ni kuwafanya wachache watoe riziki kwa ulimwengu na wanufaike kwa matunda yake. Filosofia ya utandarizi ni kuwazuia binadamu kujiongoleza maisha. Tena uhuru wa kujitegemea wa jamii watekwa nyara na mtazamo wa ulimwengu kama jamii ya namnna moja.
Mbinu zenye dhurufu kwa siri zimechukua kiti cha ujeuri mkali zaidi kama ule wa utumwa, ukoloni na wa siasa nyingine mbovu kama zile za Taylor na Stakhanov.
Tangu zamani sana, wanaume na wanawake wamepigania ustahili wa binadamu, wamejitahidi ili mtu asiwe mbwa mwitu kwa mwenzake.
Siku hizi, lengo hili ambalo mara kwa mara limewahi kuzaa matunda manono linataabikwa, linasimamishwa na kupigwa vita na wale wanaojiteua kuwa "viongozi wa dunia" (kama wanavyojiita wenye kuhuzuria mkutano wa Davos). Msimamo huu unarudisha matendo ya karne ya 19 sasa mwanzoni mwa karne ya 21.
Mwongozo wetu ni wa kimataifa. Namna yetu ya kupinga mashirika ya kimataifa,
hasa hasa Muungano wa Ulaya na Shirika la Biashara Ulimwenguni haiwezi kamwe
kufananishwa na ubinafsi wa kiuzalendi. Wakati tunaposhambulia ukiritimba na
ukosefu wa uangavu wa mashirika haya, tunaiunga mkono demokratia, hatutetei
mfumo wa serikali-taifa. Si serikali-taifa ambayo inahodhi peke yake uhuru wa
nchi. Uhuru huu unapaswa kujithibitisha kwenye madaraja ya chini ama ya juu ya
serikali-taifa. Vile vile, heshima yetu kwa anuwai haina uhusiano wowote ule na
upunguo wa thamani ya kila jamii. Twakuwa miongoni mwa wale wanaokubali umuhimu
kamili baina ya kubaki na mizizi nyumbani na kufungua milango kwa ulimwengu.
Jean Jaurès alishangaa na kusema : "Ukimataifa mchache wakubeba mbali
na nchi ya asili yako, ukimataifa mwingi wakurudisha nyumbani". Nchi ya
asili, kufuatana na maoni yetu, kama alivyoandika Cicero " pahali
unapojihisi vizuri".
Upinzani wa utandarizi husababisha shughuli nyingi, shughuli zote hizi zikiwa
muhimu na kutimizana. Tuliamua kuchagua ile inayotangaza maripoti ya wataalamu
ili watu wengi wazijuwe, ziwahimize kwa kazi inayohitajika na ziwasaidie
kuendeleza kazi hii. Watafiti
wengine wamefuata mikondo ya njia hii. Twataja kazi za wenzetu hawa, kama zile
za matimu bora sana ya Corporate Europe Observatory) na Focus on Global South
(Bangkok). Kwa upande mwingine, hatutasita kushirikiana na wengine ili kazi yetu
ifaidike.
Nyanza za kazi zi za
utata. Utata huu unakuwa mgumu zaidi kutokana na usiri pamoja na ukosefu wa
uangavu wa jinsi uamuzi unavyofanywa. Ni kwa hiari maandiko yanayoonyeshwa kama
yenye kuongoza maisha yetu hayafahamiki kwa wengi kutokana na msamiati
unaotumiwa pamoja na mifumo ya sentensi zenyewe. Kama vile maandishi haya
nanavyoandikwa kisiri, yanazidisha ukosefu wa uangavu wa wenye kutoa uamuzi.
Tulipofungua Ofisi ya
Utafiti, Ushauri na Maarifa kuhusu Utandarizi, tulikuwa na nia ya kusimbua
maandiko, mapatano na maamuzi, nia ya kufasiri na kujulisha wote kazi hizi. Vile
vile, tuna lengo la kueneza ufahamu huu kwa wale ambao hawafikiriwi, hasa hasa
wakaaji wa nchi za kusini.
Kazi yetu i mchango. Tu
tawi la kundi la kazi pana zaidi, kundi lishughulikalo na nyanja tofauti.
Twaunga mkono kabisa utofauti huu. Nguvu za Ukimataifa wa wananchi zasababishwa
na kuwa ukimataifa huu watupilia mbali mfumo wa zamani wa maukimataifa
yaliyokuwa yanalazimisha wote kiimla kufuata mtindo wake. Sote twajua mtindo huu
ulivyofeli. Tunategemea kuwa ndani ya ukimataifa Wishi letu ndani ya ukimataifa
ni kutia mkazo kwenye mashabaha yake na kufuata mara chache iwezekanavyo
masharti ya muundo na mpangilio wa mashirika.Kazi inayofaa yaweza kukamilika
bila kukana utofauti baina ya watu. Mbinu hii i bora kuliko kufuata mfumo wa
zamani unaotegemea tu uongozi wa juu. Hatujali ikiwa watu fulani husisitiza
tofauti baina maoni yetu na yao, bila kutegemea uhususiano unaotukalibisha.
URFIG imekabidhi msaada mnono wa OXFAM-Solidarité ya Ubejiji, na Institut pour la Relocalisation de l'Economie ya Ufaransa. Mashirika mawili mengine, yaani Fondation France Liberté na Goldsmith Fondation yametuunga mkono. Profesa Pierre Bordieu pia ametutia moyo. Bila mashauri yake kazi hii haingedhihirika bila mchango wa Profesa Bordieu. Tunashukuru vile vile watoji msaada wawili waliotusaidia kwa moyo mkunjufu. Hawa hawakutaka majina yao yatajwe.
Kwa hawa wote twasema, akhsanteni.
Timu
yetu
| - Brussels - | - Paris - | - Geneva - |
|
Raoul Marc JENNAR |
Jamila EL IDRISSI |
Vincent LEGRAND |
| MWENYE SHAHADA YA TATU YA FANI YA SAYANSI YA SIASA | MWENYE SHAHADA YA KWANZA YA FANI YA FALSAFA | MWENYE SHAHADA YA PILI YA FANI YA SIASA |