URFIG – Habari za Afrika

 

 

Bunge la Kenya lapitisha muswada wa sheria

kuhusu madawa ya UKIMWI

(12 Juni 2001)

 

NAIRIBI (Reuters) – Jumanne, Bunde la Kenya limepitisha muswada wa sheria wenye utata. Muswada huu ulipingwa na makampuni makuu ya dawa yanayoruhusu nchi hii ya Afrika ya Mashariki kuingiza na kutengeneza madawa rahisi.

Wabunde, wote kwa pamoja, wamepiga kura na kukubali muswada wa sheria unaohusika (Industrial Propeties Bill 2001). Hivi, walilegeza mamlaka ya makampuni makubwa ya madawa, yenye hati za haki zinazothaminiwa sana juu ya madawa tofauti, kukiwamo yale yanayopunguza ukali wa virusi vya UKIMWI.   

Wahamasishaji wanaopiga vita UKIMWI wanasema kwamba kufuatana na muswada huu, zaidi ya miliyoni 2.2 za Wakenya wenye virusi vya UKIMWI watapata madawa ambayo, katika Nchi za Magharibi, yalipunguza vifo vinavyosababishwa na UKIMWI kwenye kiwango cya asilimia 75.

Kenya ni nchi ya pili ya kiafrika inayopitisha muswada wa namna hii. Mnamo mwezi wa Aprili, nchini Afrika ya Kusini, makampuni ya madawa yalipoteza nguvu wakati yaliamua kuacha ushtaki mahakamani dhidi ya muswada wa sheria unaofanana na huu.

"Hii ni siku kuu, siku kuu sana", aliambia Reuters Bwana Sam Ongeri, Waziri wa Huduma za Afya kwa Wananchi. "Wakenya wanaweza kutabasamu, sasa wana uwezo wa kujinunulia madawa rahisi, bali bora".

Walakini itachukua muda kidogo kabla ya madawa rahisi haya kuingizwa nchini Kenya kwa jumla. Inabidi muswada urudi bungeni na kusoma upya. Pale marekebisho madogo madogo huenda yatajadiliwa. Bali kiini chenyewe cha sheria hakiwezi kubadilishwa. Baadaye, ridhaa ya rais itahitajika.        

Kufuatana na muswada wa sheria, Kenya itayapa notisi ya miezi sita makampuni ya madawa ya kimataifa yenye kumiliki hati za haki, ikiwa inataka kutoa kwa makampuni mengine vibali vya kuingiza ama kutengeneza madawa ya ainasafu.

Makampuni yanaogopa kwamba nchi nyingine za Afrika zinaweza kufuata nyayo za muswada huu na kuondoa faida ambayo, kwa niaba ya makampuni haya, ni muhimu kwa utafiti wa madawa mapya. Katika bara hili watu miliyoni 25.3 wana virusi vya UKIMWI.

Lakini, kwa upande mwingine, Bwana Ongeri anadhani makampuni ya madawa hayangelikuwa "na busara" yangelishtaki kwenye mahakama ya Kenya muswada huu. "Haingeenea kwenye hali ya taifa", alisema Waziri.