HABARI ZA DOHA

 

SHIRIKA LA BIASHARA ULIMWENGUNI - TAARIFA YA DOHA

 INGAWA KUNA BREKI, MPANGO WA BIASHARA YA KIMATAIFA WAENDELEA KUANDALIWA

 (Dr Raoul Marc JENNAR , 21 novemba 2001)

 

Kama ilivyokuwa katika mkutano wa Marrakech, katika mkutano wa Doha, nchi tajiri hazikulegeza sera yake ya kulazimisha dunia nzima kufuata mfumo mkali wa huria ya kibiashara. Walakini, tangu 1994, mwishoni mwa duru ya Uruguay, wakati yalipopitishwa maafikiano mengi ya Shirika la Biashara Ulimwenguni, sera hii haikuridhisha wale wote wanaopendekeza hasa, ili umaskini upunguzike, kugawana ifaavyo mali inayozaliwa, usawa wa haki na kutovunja haki za kila jamii juu ya maslahi binafsi.

Kila mwaka, vionyesho vyote vya kiuchumi vinathibitisha kwamba huria ya kibiashara, inayopendekezwa, inanufaisha nchi tajiri peke yake. Kutowahi kuamua kitu katika mkutano wa mawaziri wa Seattle kulihimiza nchi za Kusini kupinga nia ya ubeberu wa nchi za Kaskazini. Kutokana na maendeleo thabiti, katika nyanja za ustadi, ya nchi zinazoengelea, pamoja na mshikamano wa maoni ya nchi hizi, mkutano wa Doha, ingawa ulianzisha upya duru ya biashara ya bidhaa na huduma, ulipunguza tamaa ya nchi tajiri. Bali, kazi yenyewe ya mkutano wa Marakech haikukataliwa. Hali kadhalika, itabidi kuwe na juhudi mpya zaidi, ili upinzani wa nchi zinazoendeleo uwe na msimamo imara katika mkutano wa mawaziri utakaofanyika mnamo miaka miwili. Baadhi ya dharura za nchi tajiri zinatarajika kujadiliwa katika mkutano huu.

Mkutano wa Doha ulikuwa pia somo kwa Wanaulaya wanaopigania kuwepo kwa dunia halali, inayoheshimu haki.. Dunia yote ilitambua unafiki na kuwa na ndimi mbili kwa serikali za Ulaya na Kamisheni ya Brussels. Hotuba za kiutu na ukarimu, zenye lengo la kutuliza wazalendo wema wa kiulaya na kutumia vibaya uaminifu wa baadhi ya serikali za kusini, bado hazijajithibitisha katika mapatano. Ukweli ni kwamba Ulaya unakuwa kwenye upande wa Marekani, siyo kwenye upande wa nchi zinazoendelea : sera ya kulinda viwanda vya nchini inapitishwa ikiwa tu inaridhisha nchi tajiri.

Hivyo, wajidhihirisha wajibu wa serikali 15 za kiulaya pamoja na vyama vya kisiasa vinavyoziunga mkono. Serikali zote za kiulaya, ikiwa ni ile ya Jospin au ya Berlusconi, zi pamoja katika kuunga mkono uwezo na kazi ya Pascal Lamy. Kwa bahati mbaya, kushiriki katika serikali nyingi kwa Wakomunisti au kwa wateteaji wa mazingira, hakukubadili kitu.

Kutokana na kuwa katika mkutano wa Doha wananchi hawakuweza kubadili uwezo uliopewa Kamisheni ya Ulaya na mabunge 15 ya kitaifa pamoja na serikali 15 vile vile tangu mkutano wa Seattle, inafaa zibuniwe mbinu za kutumia katika miezi ijayo. Hali serikali za kiulaya na vyama vinavyoziunga mkono zilivyoonyesha kuridhika kwake huko Doha kwatuonyesha njia ya kufuata.

NAMNA YA KUAMUA : BADO UKO UKIRITIMBA WA WATU WACHACHE

Nchi zinazoendelea zilionyesha jitihada kubwa katika kuandaa mkutano wa Doha. Jitihada hii ilionekana pia katika kufafanua mambo na kufasili maoni na mapendekezo. Nchi hizi zilijadili kidemokrasia, kinyume na Wamarekani na Wanaulaya wanaojidai kuwa waalimu wa Demokrasia. Wamarekani na Wanaulaya walitumia nguvu zote ziwezekanazo ili mkutano wa Doha uanze watakavyo, bila kujali kufuata kanuni za Shirika la Biashara Ulimwenguni.

Misimamo iliyotangazwa na nchi zinazoendelea katika mikutano mingi ya kimataifa [mikutano ya nchi za kiafrika, kundi la Afrika Karibean na Pasifika, nchi zinazoendelea, kundi la nchi 77] au katika mikutano rasmi au la ya Shirika la Biashara Ulimweguni, haikuzingatiliwa au ilikanwa. Vyombo vya habari vya magharibi viliunga mkono serikali zake vikikataa kusema kitu juu ya maoni yaliyokwenda kinyume na maoni nchi tajiri zilizotaka kupitisha kwa nguvu.

Miswada tofauti ya taarifa ya mawaziri iliyoandaliwa na Halimashauri kuu ya Shirika la Biashara Ulimwenguni ilitegemea kikashfa upande mmoja. Bila kujali uvunjaji wa kanuni za shirika hili, miswada hii haikugusia misimamo ya nchi zinazoendelea. Tangu walipofika Doha, wajumbe rasmi walilazimishwa kujadili juu ya mswada wa taarifa ulioamriwa na nchi tajiri. Inajulikana wazi kwamba unapojadili juu ya maoni ya mpinzani wako, unajiweka katika hali ya udhaifu.

Huko Doha, maandalizi ya kazi hayakujali kanuni za kimsingi za udemokrasia katika mijadala. Kinyume, sikio lilitegwa mwenye nguvu. Nguvu hizi zilitumika vile vile katika mikutano ya nchi kwa nchi baina ya nchi tajiri na nchi zinazoendelea. Ahadi, kama vile hamanisha, ilitumiwa. Watu walioteuliwa, ili waendeshe mashauriano kwa niaba ya urais, walichaguliwa katika wafuasi wa sera za nchi tajiri. Hali kadhalika, nyanja zilizochaguliwa kujadiliwa ni zile zinazozingatia mapendekezo ya nchi zizi hizi.

Nchi zinazoendelea zilipigania kuingizwa kwa mjumbe wake katika wawakilishi hawa waliojadili juu nyanja zinazopendekezwa na nchi hizi.. Ingawa mapatano yalifanyika katika makundi saba, jambo ambalo lisingeliwezekana bila kuwepo kwa ujumwe mkubwa kwa kila nchi, mashauriano haya, kama vile mikutano ya wakuu wa ujumbe, ilizipa nchi maskini fursa ya kuifanya sauti yake isikike.

Hii ni hatua nzuri iliyofanyika, kinyume na wakati wa mkutano wa Seattle, ambapo wajumbe wa nchi maskini, -ingawa wajumbe hawa walikuwa wengi kuziidi wengine-, walikuwa wanangonja vishorobani kukubaliana kwa wajumbe wa nchi tajiri waliokuwa wanaendesha mapatano kati yao.

Katika mkutano wa Doha, nchi tajiri hazingelijaribu kuweka kando nchi maskini na kujadiliana kati yake bila kupotosha mkutano kama ilivyokuwa katika mkutano wa Seattle.. Si rahisi kutenga nchi yenye biliadri ya wakaaji, kama ilivyo India. Ndiyo maana mbinu zote za ustadi wa shughli zilitumiwa.

Ilipogunduliwa kwamba nchi maskini zilikuwa na uwezo wa kulazimisha nchi tajiri kuacha baadhi ya mapendekezo yake, « mashauriano yasiorasmi » yalianzishwa upya. Mbinu hizi zilitumiwa vile vile katika mikutano ya Marrakech na Seattle, kama zinavyotumiwa katika kazi ya kila siku ya Shirika la Biashara Ulimwenguni. Mbinu hizi zajulikana kwa jina la utaani la « green room », kutokana na rangi ya awali ya chumba cha ofisi ya mkurugenzi mkuu wa Shirika la Biashara Ulimwenguni.

Chumba « green room » cha Doha kilikuwa ni « chumba kibubwa cha kirais n° 11.» Hapo ndipo kundi la wanamagharibi na marafiki zake walipokutania katika mara tofauti na wajumbe wa nchi zenye msimamo mkali kuliko nyingine. Katika usiku wa maamuzi wa tarehe 13 na 14 Novemba, mbinu hii ilitumiwa pia kwa ajili ya kuweka India kando ya wajumbe wengine. Usiku huu ndio ulioathiri mwelekeo wa mkutano wa Doha

Shughli zilizofanyika tangu juma nne saa tatu usiku na juma tano saa 11 asubuhi ziliendelea kwa kuvutia. Nchi 20 tu (juu ya 144 kutokana na kuwa Uchina na Taiwan ziliteuliwa kuwa wanachama mnamo mkutano wenyewe) zilikubaliwa kuingia katika chumba n° 11. Nchi nyingine zilizotaka kushiriki hazikukubaliwa kuingiamo. Baadhi ya nchi zilizokubaliwa kuingia ziliruhusiwa kuwakilishwa na waziri wake peke yake. Waziri hakukubaliwa kuwa pamoja na mtaalamu wa kumshauri. Wenye kuendesha shughli hizi walichanganyisha nchi zilizoshiriki wakitumia maandiko ya kujadiliwa. Ili mswada uwahi kupitishwa, washawishi walikuwa wanaahidi :msaada wa kiufundi au walitisha kusimamisha msaada huu. Mawaziri « wakaidi » hata waliogofywa na kuteswa. Katibu wa Shirika la Biashara Ulimwenguni aliunga mkono namna hii ya kutenda, bila kujali wajibu wake wa kufanya kazi kwa ajili ya wanachama wote.

Ni baada ya usiku ule ulipomomonyoka umoja kati ya nchi za kiafrika, nchi za Afrika Karibean na Pasifika na nchi maskini. Nchi za Afrika Karibean na Pasifika zilikuwa zimekubaliwa kufuata watakavyo mfumo maalum wa kibiashara, kufuatana na maafikiano ya Cotonou.

Walakini, ingawa kulikuwepo vitendo hivi vya kimafia, vitendo ambavyo havishangazi kujitokeza katika uwanja wa biashara, viitendo vilivyoungwa mkono na Serikali zetu, katika masaa ya mwishoni mwa mkutano ulioongezewa muda wa siku moja, nchi kumi zilikuwa bado na msimamo wake imara kabla ya kukutana kwa viongozi wa wujumbe. Nchi hizi zililegeza msimamo wake zilipotishwa kujibu peke yake mkutano ukifeli, kama ulivyofeli huko Seattle. India tu ndio ilioendelea kupigana vita hadi mbali iwezekanavyo. Hatimaye, nchi hii ilikubaliwa ufafanuzi thabiti juu ya mwanzo ulioahirishwa wa mapatano yahusuyo nyanja zilizoitwa nyanja za Singapore (jambo hili litarudiwa). Ndiyo maana gazeti la kifaransa « Le Monde » lilidharau nchi hii, eti « nchi hii ilijaribu kuwa kizuizi hadi mwishoni. »

Doha ilionyesha wongo wa maandiko yaliyotangazwa hivi karibuni, tarehe 09.11.2001, na gazeti Financial Times. Gazeti liliandika kwamba « mfumo wa kimataifa wenye misingi ya kikanuni unawapa maskini na wenye kukosa nguvu haki zinazofanana na zile zinazopewa matajiri na wenye nguvu ». Shirika la Biashara Ulimwenguni lakosa demokrasia. Mfumo wa Shirika hili waheshimu mwenye nguvu sio sheria. Sharti Shirika la Biashara Ulimwenguni lirekebishwe bila kukawia. Kudharauliwa kwa nchi zinazoendelea kungelihimiza nchi hizi kuomba vya kipaumbele marekebisho haya katika mkutano ujao wa mawaziri.

TAARIFA YA DOHA YENYEWE : YOTE YAMO, ISIPOKUWA MAENDELEO

Ili « Taarifa ya Doha» ieleweke vizuri, bora kukumbuka kwamba kuna aina mbili za mapatano katika Shirika la Biashara Ulimwenguni. Kufuatana na Maafikiano ya Marrakech, kuna nyanja ambazo hujadiliwa kadri kwa kudumu : kilimo, huduma na haki ya kazi za kitaaluma. Hii ndio « ajenda ya daima. » Kuwepo au kusiwepo mkutano wa kiwaziri, kuwepo duru mpya au la, mapatano katika nyanja hizi yamepangwa na yanaendelea kufanyika. Uamuzi wa mkutano wa mawaziri ndio tu unaokuwa na uwezo wa kusimamisha mapatano haya, kuyapunguzia uwezo au kuyapa mwelekeo mpya. « Taarifa ya Doha » hufafanua mielekeo ya mapatano juu ya nyanja hizi tatu.

Hivyo, dhaana yenyewe ya « duru mpya » ina sasa lengo la mapatano juu ya nyanja nyingine, totauti na nyanja hizi. Katika ratiba ya Doha kuna ajenda ya daima, kuna vile vile duru mpya ya mapatano.

Katika majira ya kuchipua jana, huko Uswidi, kulikuwepo mkutano wa wakuu wa Marekani na wa Ulaya. Katika mkutano huu serikali za shirika hili la kiuchumi baina ya nchi jirani za Atlantiki ziliwishi kuwepo kwa duru mpya kubwa ya mapatano. Mapatano ya namna hii yangeliruhusu kunafisishwa kwa nyanja mpya ambazo kawaida zina uhusiano na maisha ya kijamii. Tarehe 29 Oktoba, nchini Luxamburg, serikali 15 za kiulaya ziliunga mkono kuwepo kwa duru kubwa. Wiki chache zilizopita, huko Singapore, katika mkutano, usiokuwa rasmi wa nchi 20, kutokana na upinzani wa nchi zinazoendelea, mpango huu ulipewa jina mpya la « ajenda ya maendeleo ». Jina hili mpya halikubadili kitu juu ya mapendekezo makali ya kunafisisha biashara.

Mpango wa Doha, iwe ajenda ishirikishayo au duru mpya, si mkubwa wala wa kimaendeleo. Mpango huu unazingatia tu makubaliano machache ya nchi tajiri, bila kufungulia milango mapatano juu ya mapendekezo ya nchi zinazoendelea. Kama alivyoandika Chakravarti Raghavan katika SUNS (n° 5011 ya tarehe 16 Novemba 2001), twaweza kuita duru hili « duru la kila kitu isipokuwa maendeleo. »

Kanuni ya kwanza na ya pili za Taarifa zathibitisha uzuri wa biashara yenye uhuru wote. Kwa niaba ya wateteaji wa taarifa hii, biashara yenyewe ya namna hii ingeliboresha hali ya uchumi na maendeleo. Wote walijivuna eti wanataka kupiga vita umaskini. Neno hili liligeuka kama wimbo wa mashirika ya kimataifa (Benki ya Dunia, Sanduku la Kimataifa la Fedha na Shirika la Biashara Ulimwenguni). Jambo la kushangaza ni kwamba ni mashirika haya yaliyosababisha hali ya leo ya umaskini.

AJENDA YA DAIMA

Mapatano juu ya nyanja tatu zinazohusu ajenda hii hudumu na kuendelea kwenye makao ya Shirika la Biashara Ulimwenguni mjini Geneva. « Taarifa ya Doha » ilionyesha tu mielekeo ambayo ingelifuatiliwa na mapatano haya. Kinyume na ombi la nchi zinazoendelea, taarifa hii haikukosoa kamwe maafikiano yanayohusika.

Kilimo

Wengi mno kati ya binadamu duniani wahusika na uwanja huu, yaani wakulima wadogo wadogo. Uwanja huu wadhihirisha unafiki wa Muungano wa Ulaya na Marekani. Kila mwaka, Muungano wa Ulaya na Marekani hutumia biliardi 380 za dola ya Marekani kama lipo au msaada wa aina mbalimbali. Nchi zizi hizi, zikirejesha kwenye Maafikiano juu ya Kilimo, huzuia nchi nyingine zote duniani kusaidia kilimo pamoja na uzalishaji wa bidhaa za ulimaji (ikiwa nchi hizi zina uwezo wa kutekeleza jambo hili). Nchi hizi huzuiliwa pia kulinda masoko yake ya ndani dhidi ya mchuano huu ambao si halali.

Doha haikuwapa kitu wakulima wadogo wadogo. Wakulima hawa hawakupewa kitu juu ya kilimo, juu la kulinda rasilmali ya asili au ujuzi wa kienyeji (tazama majadiliano juu ya Maafikiano kuhusu Haki za Kitaaluma -ADPIC). HAPANA KITU. Muungano wa Ulaya ulijaribu hata kuufanya ufeli mkutano wa Doha kwa ajili ya kulinda viwanda vya ulimaji barani Ulaya. Matunda ya uzalishaji wa hali ya juu wa bidhaa za kilimo barani Ulaya yajulikana : dioxine, ng’ombe wenye wazimu, maradhi ya homa ya mifugo, uchafuzi wa mazingira wa hali ya juu.

Nchi zinazoendelea zilikuwa zinaomba kuandikwa katika maafikiano juu ya kilimo kwa sura maalum inayohusu viwango vya ushuru wa forodha ya upendeleo pamoja na uamuzi halisi juu ya ulimaji mdogo mdogo. Muungano wa Ulaya ulipinga sana ombi hili lijulikanalo kama « Development Box ».

Katika mswada wa taarifa kulikuwa kumeandikwa kwamba ingefaa « kuwepo kwa mapatano ya jumla kwa ajili ya kupungua misaada kwa usafirishaji wa bidhaa nje, na kusimamisha baadaye, hatua kwa hatua, misaada hii ». Kutokana na kuwa misaada ya Muungano wa Ulaya i tofauti na ile ya Marekani, Muungano wa Ulaya ulipendekeza na kukubaliwa kuandika usahihi kwamba kupungua misaada kungehusu « aina zote » za misaada. Walakini, kwa upande mwingine, Muungano wa Ulaya ulikubaliwa kutokuwa na maana kwa maneno « na kusimamisha baadaye, hatua kwa hatua, misaada hii » kwa sababu, kabla ya maneno haya, kuliandikwa « bila kuenda kinyume na matokeo ya mapatano yenyewe ».

Huduma

Taarifa ya Doha inathibitisha mapatano yaliopo, mielekeo iliyoamuliwa na shabaha linalofuatiliwa. Ingawa wananchi walifasiri woga wanao, hakukuwa na uamuzi thabiti wa kulinda huduma kwa umma dhidi ya haja ya unafisishaji. Aya ya 7 ya Taarifa ndiyo peke yake inayoeleza  : « Kutokana na Maafikiano ya jumla juu ya Biashara ya Huduma, tunathibitisha mara nyingine haki ya Wanachama ya kujitungia sheria kuhusu utoaji wa huduma, na kujibunia sheria mpya katika uwanja huu. »

Watu wengi huamini kuwa aya hii itaziruhusu nchi kulinda dhaana ya huduma kwa umma, hasa hasa katika nyanja za elimu na afya. Isisahaulike kwamba katika mapatano juu ya mazingira ambayo yataanzishwa hivi karibuni (tazama chini) kuna huduma kwa mazingira ambayo moja kwa moja yanawekwa hatarini na unafisishaji.

Haki za Kitaaluma (ADPIC)

Maafikiano juu ya Haki za Kitaaluma katika Biashara (ADPIC) – Fani iliyofasiriwa mno katika Sheria ya kumiliki – huenda kinyume na haki za kimsingi : haki kwa afya (A) na haki za kila jamii kwa kuwa na uhuru juu ya asilimali yake ya kiasili (B), haki hii ikiwa tena inatiliwa mkazo katika maandiko ya sheria ya kimataifa, maandiko ambayo yalipitishwa na kuidhinishwa rasmi na nchi zote. Maafikiano haya juu ya haki za kitaaluma hugusia nyanja nyingine za kumiliki kitaaluma (C).

A. Kuhusu haki kwa afya na haki kwa madawa ya kimsingi, Taarifa pekee ilipitishwa. Kupitishwa kwa taarifa hii kulitokana na juhudi ya Nchi Zinazoendelea. Nchi hizi zilikuwa na msimamo mmoja imara katika vita hivi ambavyo kikweli vilikuwa vya « kufa au kupona ».

Mnamo mwezi wa Februari wa 2000, katika Bunge la Ulaya, Kamisheni wa Ulaya wa Biashara ya kimataifa, kwa sauti ya kuamrisha, alihakikisha kwamba haki za kitaakluma (hati) haziathiri bei ya madawa.

Taarifa iliyopitishwa Doha yaonyesha kinyume. Yaliofanyika mpaka sasa yalichunguzwa. Maandiko ya Doha juu ya « Maafikiano juu ya Haki za Kitaaluma na Afya » ya hatua kubwa ya kisiasa, lakini yakosa nguvu za kisheria. Mara nyingi ukosefu huu ulitiliwa mkazo na ujumbe wa Marekani.

Matatizo yanayosababishwa na hati katika nyanja za afya ya umma na kukomesha magonjwa ya mlipuko yalitambuliwa na kukubaliwa. Nchi ziliwishi kwamba Maafikiano juu ya Haki za Kitaaluma yasizuie Wanachama wa Shirika la Biashara Ulimwenguni kutumia njia ziwezekanazo ili wapate madawa ya kimsingi.

Masharti yanayoamri nchi maskini kufuata Maafikiano juu ya Haki za Kitaaluma yaliahirishwa kwa miaka kumi. Bali nchi hizi zilikata kujifunga zikikubali uamuzi unaokwenda kinyume na uwezo wake. Hazikukubali kuwepo kwenyewe kwa hati. Mjini Geneva, kutafanyika mkutano juu ya uingizaji nchini wa madawa ya ainasafu. Mapatano haya yangelimalizika kabla ya mwaka wa 2002 kumalizika.

B. Kuhusu haki ya kila jamii ya kuwa na uhuru juu ya rasilmali yake ya kiasili na haki ya kupiga vita uharamia pamoja na hati katika uwanja wa viumbe hai, kanuni ya 19 ya Taarifa yaomba Ushauri wa Maafikiano kuhusu Haki za Kitaaluma, kuchunguza upya kanuni ya 27 :3 b, kuchunguza utekelezaji wa maafikiano yahusuyo maafikiano juu ya APIC (…) kuchunguza uhusiano baina ya haki za kitaaluma na vuimbe hai, ulinzi wa ujuzi asilia, elimu ya kitamaduni na mambo mengine muhimu… ». Ingawa aya hii yaifungulii milango mapatano mapya juu ya Haki za Kitaaluma katika Biashara kama ikivyoombwa na Nchi Zinazoendelea, yaikatai majadiliano juu ya kanuni ya 27 : 3 b), kinyume na yaliyopendekezwa na Muungano wa Ulaya.

Maendeleo kuhusu uwanja wa Haki za Kitaaluma katika Biashara (kuhusu madawa) yanayoonekana katika Taarifa ya Doha yasikiche hali ya kwamba Maafikiano haya hayatajadiliwa upya. Kutokana na matashi ya viwanda vya kimataifa vya madawa na vya bidhaa za kilimo, Muungano wa Ulaya na Marekani zakata kata kata kuwepo kwa maafikiano mapya, kinyume na yanayoombwa na Nchi zinazoendelea.. Hivyo, kazi ngumu zaidi bado haijafanyika.

C. Taarifa inatangaza kuanzinshwa kwa majadiliano juu ya kuwepo kwa mfumo wa kimataifa kujulisha na kuandika hali ya mivinyo na pombe kali. Jambo hili laweka katika matumizi kanuni namba 23 ya Maafikiano juu ya Haki za Kitaaluma katika Biashara, haliirekebishi.

DURU MPYA

Majadiliano yatafanyika tangu tarehe 01.01.2002 hadi tarehe 01.01.2005. Yataongozwa na kamati maalum. Mtutano wa mawaziri utachunguza matunda ya majadiliano haya. Uendeshaji, matunda na utekelezaji wa majadiliano haya utahusu na kufuatwa mara kwa mara na wanachama wote. Majadiliano haya yatakuwa juu ya nyanja zifuatazo :

- Haki kwa wote kwenye masoko ya bidhaa zisizo za kilimo : panahusika hapa ushuru na bei za bidhaa viwandani. Nchi zinazoendelea, hasa hasa zile za kiafrika, zilikuwa zimependekeza kutokuwepo kwa majadiliano kabla ya uchunguzi thabiti juu ya athari ya kushusha ushuru na bei kwa kuendeleza viwanda katika Nchi Zinazoendelea. Sauti ya nchi hizi kaikusikika. Kama hawaangalii makini, majadiliano juu ya uwanja huu huenda yakasababisha upanishaji mkubwa wa uhuru wa kibiashara, katika nyanja zihusuzo maendeleo ya kudumu.

- GATT 1994 (yaani maafikiano yaliyofanywa na GATT ya awali hadi 1994) : mapatano yatahusu utekelezaji wa kanuni zilizopo, hasa hasa katika uwanja wa kimisaada (kwa mfano uvuvi) na wa biashara ya kimajimbo.

- Mazingira : majadiliano yatafafanua uhusiano baina ya kanuni zilizopo ndani ya Shirika la Biashara Ulimwenguni na maafikiano ya kimataifa juu ya mazingira, walakini majadiliano haya hayatahusu nchi ambazo hazikutia saini kwenye maafikiano haya. Hivyo, Marekani bado iko na uhuru wa kutenda itakavyo na kuamuru wengine kufuata kanuni wasizozitaka. Isitoshe, kufuatana na inavyoandika, aya yenyewe yafasili, bila kutaja bayana, utiaji fora wa kanuni za Shirika la Biashara Ulimwenguni katika kanuni nyingine zote za Sheria ya Kimataifa. Hali kadhalika yashawishi kutounga mkono maafikiano ya kimazingira. Kufuatana na Taarifa, majadiliano ya kimazingira yatahusu « kupunguza au kufuta vipingamizi, vihusuvyo bei au la, juu ya bidhaa ama hukuma katika uwanja wa kimazingira. » Milango imefunguliwa ubinafsishaji kimazingira wa huduma za kiuma (maji, nguvu, mbolea,…). Kinyume, bali ya kuchunguzwa, mapendekezo yahusuyo vyeti vya kimazingiza yaliwekwa mikononi mwa kamati maalum. Umuhimu wa maendeleo ya kudumu haukufafanuliwa kama kipingamizi kwa uenezaji uhuru wa kibiashara.

- Utekelezaji. Hapa siyo majadiliano yenyewe juu ya nyanja mpya yanayohusika, bali mapatano juu ya namna ya utekelezaji wa maafikiano yaliopo. Nyingi mno kati ya Nchi Zinazoendelea zilikataliwa ombi lake kuchunguza upya maafikiano yaliopo. Msimamo wa nchi tajiri juu ya Maafikiano katika uwanja wa vitambaa na nguo haukugusiwa. Wala mbinu za nchi tajiri za kushusha mara kwa mara bei kwa ajili ya faida zake hazikugusiwa.

- Marekebisho ya kanuni za usuluhisho wa migogoro. Mapatano haya ndiyo peke yake yaliyohusu maafikiano yaliopo na jinsi Shirila la Biashara Ulimwenguni linavyofanya kazi yake. Kinyume na nyanja nyingine za duru mpya, mapatano haya yatapaswa kumalizika mwezi Mei 2003. Ingawa haiwezekani kujua jinsi mapatano yatakavyoendeshwa, ni vizuri kuwa kulikuwepo na uwezo wa kuchunguza upya muundo uliopo, ambao wengi waliupinga.

Katika usiku wa tarehe 13 na 14 novemba kulijadiliwa aya zifuatazo za Taarifa (20, 23, 26 et 27). Mwanzoni mwa mkutano, Nchi Zinazoendelea ziliwahi kupitisha pendekezo lake la kuahirisha majadiliano ya nyanja hizi kwenye mkutano wa tano utakaofanyika katika mwaka wa 2003. Walakini, kutokana na nguvu zilizotumiwa na Muungano wa Ulaya, nyanja hizi ziliandikwa katika ratiba ya duru mpya, tofauti ikiwa tu kwamba, kinyume na nyanja nyingine, mapatano juu ya nyanja hizi yataanza « baada ya mkutano wa tano wa mawaziri, kufuatana na uamuzi utakaochukuliwa juu ya namna ya kuendesha mapatano. »

Kutokana na kazi iliyofanywa na India, rais wa mkutano aliandika kwamba : « Ningelipenda kuandika kwamba baadhi ya wajumbe walipendekeza kufasili zaidi aya za 20, 23, 26 na 27 za mswada taarifa. Kutokana na kuwa katika mapatano haya kunahitajika kuwepo kwa « makubaliano dhahiri » mnamo mkutano wa 5 wa mawaziri, msimamo wangu ni kwamba ni bora kuchukua uamuzi dhahiri kabla ya kuanzishwa kwa mapatano juu ya biashara na utegaji uchumi, biashara na sera za mchuano, uangavu na soko za raia, kulahisisha biashara. Kutokana na hali hii ya mambo, kila mwanachama angelikuwa na uwezo wa kuchukuwa msimamo imara. Hivyo, makubaliano dhahiri yatawahi kuwepo baada ya mkutano wa 5. »

Yaani, katika mwaka wa 2003, ikiwa Mwanachama fulani hakubaliani na wengine, mapatano juu ya nyanja hizi nne hayataweza kuanzishwa. Bila shaka, Marekani na Muungano wa Ulaya zitasisitiza kwamba msimamo huu wa rais hauna maadili ya kisheria, kinyume na Taarifa yenyewe. Wanasheria huenda wakaamua. Usahihi huu wa rais wa mkutano uliandikwa katika katika Taarifa ya Doha, na hakuna mashaka juu ya uthabiti wa taarifa hii. Kadhalika, hakuna yeyote yule ambaye angelijua mkutano ungelimalizika je, bila usahihi huu uliopendekezwa na rais kabla kupitishwa kwa taarifa yenyewe. Licha ya mjadala huu juu ya sheria, kunakuwepo msimamo wa kisiasa wa kutoamuru lolote kwa nchi yoyote ile, kabla ya kuanzisha mapatano juu ya nyanja hizi.

Nyanja nyingine ambazo hazitajadiliwa, (biashara ya kielektroniki, uchumi wa viwango vya chini, madeni na fedha, kubadilishana ufundi sanifu, ushirikiano wa kiufundi na kuimarisha uwezo) zitachunguzwa na makundi ya kazi ya Shirika la Kazi Ulimwenguni.

Kifupi, ingawa muundo na kanuni za Shirika la Biashara Ulimwenguni bado hukandamiza Nchi Zinazoendelea, nchi hizi zimeanza kutetea haki zake. Mapatano yataendelea, na yataanzia kwenye nyanja mpya.  Kazi yote itafanyika mjini Geneva. Vita vikali na virefu vitahitakjika ili kuwepo biashara kwa ajili ya jamii, bali jamii kwa ajili ya biashara.

 

Dr Raoul Marc JENNAR

Mtafiti kwenye Shirika Oxfam Solidarité (Brussels) na URFIG (Brussels-Paris-Geneva)

21 novemba 2001

 

OMC : la Déclaration de Doha - MALGRE DES FREINS, L’ORGANISATION COMMERCIALE DU MONDE  SE POURSUIT (Dr Raoul Marc JENNAR, 21 novembre 2001)