HABARI ZA DOHA

 

HABARI KUTOKA DOHA (1) - 09 novemba 2001

  Shirika la Biashara Ulimwenguni - Mkutano wa 4 wa Mawaziri

VITA KUSINI

 

Leo ijumaa, kulianzishwa mkutano ambao wapaswa kuendelea na kazi iliyosimamishwa miaka miwili iliyopita, mjini Seattle. Kosa kubwa larudiwa

 

Kama ilivyokuwa katika mwaka wa 1999, nchi tajiri, zikiongozwa na Muungano wa Ulaya, zatetea kuwepo kwa duru mpya ya mapatano, kwa ajili ya kupanisha nyanza ambazo zi mikononi mwa shirika la Biashara Ulimwenguni na tawi lake linalokuwa na wajibu wa kutatua migogoro. Tawi hili ndilo peke yake duniani linalokuwa na uwezo wa kuamrisha nchi kadha kubadili katiba yake, sheria na kanuni zake, ikiwa katiba, sheria na kanuni hizi zinazuia mabadilishano huru ya biashara kama yanavyofafanua na maafikiano ya Shirika la Biashara Ulumwenguni. Ikumbukwe kwamba maafikiano haya yalitokana na usuluhishi wa serikali na kuidhinishwa rasmi na mabunge.

 

Serikali 15 za Kiulaya, kukiwamo wakomunisti wa Kifaransa na mafashisti wa Kiitaliano, zimempa Bwana Pascal LAMY, ambaye ni mpatanishi wa Kiulaya, uwezo wa kudadiliana ambao ni ule ule wa 1999. Waliongezamo kinafiki, kama ilivyo kawaida katika taarifa za Ulaya, kwamba mpatanishi « angezingalia mapendekezo ya nchi zinazoendelea ». Bali jambo hili haligusiwi kamwe, Wanaulaya wanapendelea zaini ushirikiano wao na nchi tajiri nyingine.

 

Ukweli wa mambo ni kuwa nchi tajiri zapiga vita nchi za kusini, zikiamrisha sera za uhuru wa mabadilishano ya kibiashara na kulinda maslahi yake ikiwa uhuru huu wa kibiashara wakuwa kipingamizi kwa hali yoyote ile kwa manufaa ya nchi hizi tajiri (maafikiano kuhusu kilimo, maafikiano kuhusu vitambaa vya nguo, maafikiano juu ya haki za kitaaluma). Isitoshe, nchi hizi zaamrisha kwa nguvu kanuni na kuweka vikwazo kwa kanuni hizi, bali hukataa kuchunguza athari za kanuni hizi kijamii na kiuchumi, na hutaka kusambaza sera zake juu ya uhuru huu wa kibiashara bila kuchunguza maoni ya nchi zinazoendelea.

 

Kila mara Ulaya na Marekani hutumia maneno kama demokrasi na haki kisheria kwa ajili ya kutekeleza mipango yake. Kinyume, nchi hizi hazisiti kuvunja kanuni zilizojibunia. Katika Shirika la Biashara Ulimwenguni hakuna mabadiliko yaliyofanyika tangu mkutano wa Seattle, ikiwa ni juu ya uangavu na demokrasia katika utoaji wa uamuzi. Nchi hizi hazikutoa somo kwa yaliotokea Seattle. Hali kadhalika, mambo yaliharibika zaidi.

 

Katika Shirika la Biashara Ulimwenguni, kwa kawaida, wanachama wote hupaswa kukubaliana kabla ya kutoa uamuzi wowote ule. Kinyume, msingi huu maalumu hudharaulia.

 

- Nchi ambazo hazitangazi msimamo wake (kutokana na kuwa hazina ubalozi mjini Geneva ama ikiwa idadi na utaalam wa wafanyakazi wake havitoshi kwa kufuata mikutano ambayo i mingi kila siku kwenye Shirika la Biashara Ulimwenguni) huchukuliwa kama vile zingeunga mkono jambo linalojadiliwa.

 

- Majadiliano yanayobuniwa kutokuwa rasmi, baina ya nchi tajiri pekee yake, ama yanayoshirikisha mara kwa mara nchi nyingine chache kutokana na jambo ya kujadiliwa, yaliendelea kufanyika, tena yana utaratibu dhahiri. Wengine hawana budi kufuata mapendekezo yanayotolewa na majadiliano ya namna hii, bila kupewa uwezo wa kueleza maoni yao

 

- Katika maandalizi ya mkutano wa Doha, mbinu zaidi zilibuniwa :

 

- majadiliano makubwa ambayo si rasmi yanashirikisha aina zote za nchi. Wanachama ambao hawakualikwa katika aina hii ya mikutano wanakataliwa kushiriki. Nchi zenye msimamo imara (baada ya mkutano wa Singapore zawekwa kando. Nchi tariji zilifurahishwa na kuwa ziliwahi kuweka kando India, kama vile ingeliwezekana kuweka kando biliadi ya watu)

 

- Msingi wa « makubaliano ya wote kabla uamuzi » katika Shirika la Biashara Ulimwenguni uliachiliwa. Nafasi ya kanuni hii ya makubaliano haikuchukuliwa na uamuzi wa wengi, bali na imla ya Rais wa Halmashauri Kuu ya Shirika la Biashara Ulimwenguni. Mswada wa taarifa ulioandikwa kwa ajili ya mawaziri wanaokutania mjini Doha uliandaliwa na Rais wa Halmashauri Kuu pamoja na Mkurugenzi Mkuu, wakisaidiwa na Quad, yaani ushirikiano wa nchi tajiri (Muungano wa Ulaya, Marekani, Japani, Canada).

 

Mswada wa kwanza ulikuwa umekasirisha nchi zinazoendea. Ndani yake kulikuwa kumetajwa mapendekezo yote ya nchi tajiri, walakini mswada huu haukuzingatia hata kidogo maoni ya nchi zinazoendelea.

 

Tarehe 27 Oktoba mswada wa pili ulitangazwa. Kimsingi, haukutofautiana na mswada wa kwanza. Mnamo mkutano wa tarehe 31 Oktoba, nchi 22 kutoka kusini zilionyesha upinzani wake dhidi ya mswada huu. Miongoni mwa nchi hizi kuna Misiri na India, pamoja na Tanzania ambayo ilitangaza msimano wa nchi zinazoendelea.Vile vile kulikuwemo Zimbabwe ikisimamia kundi la nchi za kiafrika. Wakati huu, kama ilivyotakwa na Ulaya na Marekani, nguvu zikaanza kutumiwa. Rais wa Halmashauri Kuu ya Shirika la Biashara Ulimwenguni alituma mswada wake ili ujadiliwe na mawaziri katika mkutano wa Doha, bila kuonya kwamba dhiidi ya mswada huu kuna upinzani, ukosoaji na marekebisho. Aliandika tu kuwa mswada huu haukuwa uamuzi wenyewe wa Halmashauri Kuu. Tendo hili lilikuwa kinyume na maoni ya nyingi kati ya nchi zinazoendelea, pamoja na Nigeria. Nchi hii iliandika barua rasmi ya malalamiko, bali barua hii haikuwekwa katika nyaraka zilizotayarishwa kwa ajili ya mkutano wa mawaziri.

 

Hivyo, mswada uliopendekezwa na nchi tajiri, ingawa Wanaulaya wanaonyesha kusita kidogo juu yake, u waraka rasmi uliotangazwa kwa ajili ya mkutano ambao sasa unaanza

 

Isitoshe, sheria inayoongoza Shirika la Biashara Ulimwenguni inaendelea kuvunjwa. Tangu jana, kila mmoja kwa upande wake, Muungano wa Ulaya na Marekani zinakutania hapa Doha na kila moja kati ya nchi zinazoendelea. Bila shaka lengo la mikutano ya namna hii si la kutaka kujua tu maoni ya nchi hizi...

 

Hatua mpya katika ukosefu wa demokrasia ilidhihirishwa na jinsi viondozi wane wanavyotenda (Harbinson, Rais wa Halmashauri Kuu, Mike Moore, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Ulimwenguni, Pascal Lamy, Mpatanishi wa Kiulaya na Robert Zoellick, Mpatanishi wa Kimarekani). Mara sita viongozi hawa walifanya mikutano ya majadiliano isiyo rasmi juu ya nyanja zinazokuwa muhimu kwao. Uongozi wa makundi haya ya kikazi uliwekwa mipononi mwa nchi ambazo hazipingi duru mpya.

 

Maandamano ya maNGO’s katika sherehe za kufungua rasmi mkutano, wito ukiwa « no voice at the WTO », unapewa uhaki wake na kuwa sauti ya kusini pamoja na ile ya maNGO’s yanayotetea nchi zinazoendelea haikusikika (idadi ya maNGO’s yaliyoruhusiwa kushiriki ilipunguzwa sana : zaidi ya 200 wakati mashirika yenyewe huziidi 400).

 

Yaliofanyika kwenye siku hii ya kwanza hayaturuhusu kudhani yatakuwaje matunda yatakayozaliwa na mkutano huu. Kutataa kwa nchi za Ulaya kwa kurekebisha maafikiano juu ya haki za kitaaluma (hasa hasa juu ya haki kwa madawa ya kimsingi) kungepanua zaidi shimo. Walakini watu hufikiri kuwa nchi zinazoendelea zingeweza kuunga mkono duru mpya, ikiwa zinakubaliwa marekebisho zinayoyapendekeza. Hali hii ya mambo itaathiri sana kazi ya siku zijazo. Kutakuwepo makubaliano ama hakutakuepo kitu. Huenda pia, kwa ajili ya heshima, wenye kushiriki kwenye mkutano watakubaliana juu ya duru mpya ambayo haina kitu ndani yake.

 

Kutoka Doha,

Raoul Marc Jennar

09 novemba 2001