HABARI ZA DOHA
HABARI KUTOKA DOHA (2) - 10 novemba 2001
Shirika la Biashara Ulimwenguni - Mkutano wa 4 wa Mawaziri
NCHI ZA KUSINI ZARUDI NYUMA
Katika siku ya pili ya mkutano wa mawaziri wa Shirika la Biashara Ulimwenguni hotuba zilianza kutolewa hadharani. Vile vile ilianza mikutano juu ya nyanja sita ambazo imeamua zingejadiliwa kila moja kwa upande wake.
Mawaziri wa nchi tajiri wametetea kuwepo kwa duru mpya ambayo angalau ingechunguza nyanja zinazojulikana kwa jina la nyanja za Singapore (utegajiuchumi, sera ya mchuano, masoko ya umma na urahisishaji wa biashara).
Mawaziri hawa walitangaza kuwa mswada wa taarifa haukukubaliwa na wanachama wote wa Shirika la Biashara Ulimwenguni. Wengi miongoni mwa mawaziri hawa walisisitiza umuhimu wa kulegeza namna ya kufuata Makubaliano yanayohusu haki za kazi za kitaaluma (TRIPS).
Nchi ya Ufaransa, kwa upande wake, ilitetea sera ya Ulaya juu ya kilimo.
Bali nchi za kusini zilistaajabisha. Hotuba zilitengana na zile za mabalozi wa nchi hizi huko Geneva, wakati wa majadiliano juu ya mswada wa taarifa. Ingawa mawaziri wa nchi za kusini walisisitiza kwamba duru mpya haizingatii mapendekezo ya nchi hizi, ingawa nchi hizi zilitangaza kwamba hazitaki kujadiliana upya juu ya nyanja zilizojadiliwa huko Singapore, ingawa nchi hizi zilisisitiza kwamba lazma ufanyike bila kukawia utathmini wa maafikiano yaliyopo, jinsi zilivyo hutuba za viongozi hawa zinaonyesha kwamba wanasita, kwamba hawana msimamo imara kama ilivyo huko Geneva.
Bila shaka, kinyume na mabalozi ambao kila siku wanafuata yanayofanyika kwenye Shirika la Biashara Ulimwenguni, mawaziri hawaoni kabisa ukweli wa mambo juu ya mapatano ya namna hii.. Walakini hali hii ya mambo haitoshi kwa kufasiri yote. Kuna ishara zinazothibitisha kwamba vishawishi vya kashfa vinavyofanya kwa nguvu na Marekani pamoja na Muungano wa Ulaya vyaanza kuzaa matunda.
Kwa mfano, alipofika tu Doha baada ya ziara yake huko Washington na Brussels, waziri wa Biashara wa Nigeria aliwafukuza wawakilishi wa maNGO’s ambao walikuwa katika ujumbe wa nchi yake.
Kwa upande weke, waziri wa biashara wa Kenya, katika mkutano wake na wanahabari ambamo angelitangaza waraka nzuri iliyoandikwa na nchi za ACP, hakutetea waraka yenyewe, bali alitukuza Shirika la Biashara Ulimwenguni, viongozi wake na jinsi mambo yanavyotendeka ndani yake siku hizi.
Alionyesha woga mkubwa alipofika kwenye sentensi ya nchi za ACP inayolaumu vishavishi vya nguvu vinavyotumiwa na nchi tajiri.
Waziri wa Biashara wa Tanzania ambaye ni spika wa nchi zinazoendelea aliwishi mafanikio kwa mkutano na kutoa maelezo zaidi juu ya upinzani dhidi ya duru mpya. Maelezo haya yanarahisishia kazi watetezi wa duru hii.
Hotuba hizi zi mbinu itakayo tumiwa baadaye ? Mbinu za kidiplomasia ? Ni mapema sasa kutangaza ushindi wa nchi tajiri na kushindwa kwa nchi za kusini. Kama alivyosema mwanabalozi wa kibelgiji, tu bado mwanzoni mwa mkutano. Jambo ambalo ni muhimu ni kwamba nyanja sita zitatowa mwanga
Kutoka Doha
Raoul Marc Jennar
10 novemba 2001
Dr Raoul Marc JENNAR
Dr Raoul Marc JENNAR
Mtafiti kwenye Shirika Oxfam Solidarité (Brussels) na URFIG (Brussels-Paris-Geneva)
Site Web : www.urfig.org