HABARI ZA DOHA

 

 

HABARI FUPI KUTOKA DOHA (2)

 Shirika la Biashara Ulimwenguni - Mkutano wa 4 wa Mawaziri

VITA VYAENDELEA KUSINI

 

Kinyume na niliyoyaandika hapa awali, mengi yalifanyika katika usiku uliopita, kuhusu mapatano juu « Taarifa ya Doha ».

 

Makundi 450 ya wenye mali wanaokuwa hapa Doha yalifanikiwa kushawishi wajumbe wa nchi tajiri na wa Kamisheni ya Ulaya. Wenye mali hawa walikuwa wanaogopa kushindwa mara nyingine juu ya uwanja wa madawa. Wala hawakutaka kuwepo kwa duru ndogo ya mapatano.

 

Mswada wa 4 wa taarifa, uliojadiliwa na kijikundi kidogo cha nchi tajiri ulipewa wajumbe. Mswada huu unatangaza kuwepo kwa duru mpya kubwa inayotetea biashara. Inaonekana kuwa nchi zinazoendelea haziwezi kupinga mswada huu. Hatudhani kwamba huenda nchi hizi zitakataa mswada huu katika mkutano wa kilele wa mwisho.

 

Mapatano yataanza, huenda sasa hivi, huenda mnamo mwaka wa 2003, juu ya :

 

- kilimo, bila kuwa sasa kipingamizi kwa msaada wa usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi, wala bila kukubali « sanduku la maendeleo » ;

 

- kitegauchumi : kunatarajiwa tangu sasa kurudi upya kwa maafikiano ya kimataifa juu ya kitegauchumi ;

 

- sera ya mchuano, masoko ya umma na urahisishaji wa biashara (nyanja tatu zaidi za Singapore) ;

 

- haki kwa masoko ya bidhaa zisizo za kilimo (kupunguza bei za viwanda ambazo zasumbua nchi zinazoendelea) ;

 

- Huduma (kuendelea na mapatano yanayofanyika hupo Geneva) ;

 

-Uhusiano baina ya maafikiano ya kimataifa juu ya mazingira na kanuni za Shirika la Biashara Ulimwenguni. Mapatano haya hayatahusu nchi ambazo hazijaunga mkono maafikiano haya juu ya mazingira. Ni kusema kwamba nafasi muhimu ilipewa kanuni za Shirika la Biashara Ulimwenguni.

 

Kanuni ya tahadhari hayijaidhinishwa; maafikiano ya Kotonu, hadi leo, hayajapewa mkengeuko unaohitajika ili yaweze kutumika.

 

Duru ambayo huenda itaanzishwa i mbali kuwa duru ya kimaendeleo. Maendeleo juu ya sera kuhusu madawa haiwezi kuficha udhaifu wa kisheria ambao hapa Doha ulikumbushwa mara nyingi na wajumbe wa kimarekani.

 

Jamii zote za dunia zinaamrishwa kufuata mipango ya nchi tajiri.

 

Vita dhidi ya nchi za kusini.

 

Kutoka Doha,

Raoul Marc Jennar

14 novemba 2001, saa 6 na 15

 

Dr Raoul Marc JENNAR

Mtafiti kwenye Shirika Oxfam Solidarité (Brussels) na URFIG (Brussels-Paris-Geneva)

Site Web : www.urfig.org