HABARI ZA DOHA
HABARI ZA DOHA (3) - 12 novemba 2001
MIKONONI MWA UKIRITIMBA WA WATU WACHACHE : ULAYA ULISAIDIA
Ukiritimba wa kijikundi kinachoongoza Shirika la Biashara Ulimwenguni (Mwanaulaya Lamy, Mmarekani Zoellick, Mkurugenzi Mkuu Moore na Rais Harbinson – katika kijikundi hiki cha watu wane hakuna mwakilishi wa nchi zinazoendelea.) uliamua pekee yake juu ya jinsi mapatano yatakavyoendelea.
« Warahisishaji » sita, wanaojulikana kama « marafiki wa urais », waliteuliwa ili wachunguze nyanja sita zilizochaguliwa kwa nguvu. Nyanja hizi zilichaguliwa kabla ya kutafuta maneno ya ainasafu ya kufasili nyanja zinazohusika katika mswada wa taarifa. Kijikundi hiki cha viongozi kina uhuru wote wa kuandaa mashauriano (kuandaa mikutano ama kutaka ushauri wa wajumbe au wa makundi ya wajumbe wanaojichagulia).
Ikiwa kijikundi hiki kinataka kuandaa mikutano, kila ujumbe unaokuwa pale hauna zaidi ya dakika tatu kabla ya kueleza maoni yake. Mikutano hutangazwa kwenye televisheni. Matangazo haya hutumia maneno yasiyoeleweka. Kuna mara ambapo hata chumba cha mkutano hatijajwi (wajumbe wa nchi zinazoendelea walionekana wakitafuta bila mafanikio pahali pa mkutano). Kama itakavyoelezwa hapa baadaye, nyanja zilizochaguliwa hazihusu maswali muhimu kwa nchi zinazoendelea. Hali kavyalika, « warahisishaji » wote wanahesabika miongoni mwa watu wanaotetea kuwepo kwa duru mpya.
Kasoro hii ilielezwa mwanzoni mwa mkutano, bali urais haukutaka majadiliano. Nchi zilizoweza kueleza maoni yake, ingawa maoni haya hayakuzingatiwa, ni India, Zimbabwe, Jamaica, Bangladesh, Uganda na Pakistan. Hivi ndivyo ilivyo demokratia inayotetewa kwenye Shirika la Biashara Ulimwenguni na serikali 15 za kiulaya !
Baada ya siku hizi mbili za majadiliano ya namna hii, inaonekana kwamba mapatano yenyewe yanaanza, bila huruma, hakuna kupana zawadi. Tahfifu huku yaita tahfifu kule. Hakuna yeyote awezaye kubuni mambo yatakuwaje mwishoni mwa mkutano, ingawa bila shaka kutakuwepo na taarifa fulani ya mawaziri mwishoni. Kuhusu ujumbe wenyewe wa taarifa hii, inakuwa bado mapema kusema kitu. Walakani inaonekana wazi kwamba taarifa hii haitatangaza ile duru kubwa inayohitajiwa na serikali za kiulaya.
KILIMO ; Mrahisishaji : waziri wa biashara wa Singapore
Mikutano miwili imeandaliwa. Uwanja wa kilimo ndio unaoogofya wale wanaogopa kuwepo kwa Seattle mpya. Kinyume na yanayofikiriwa, wanaulaya hawana msimamo imara juu ya faili ya kilimo. Faili hii yatenganisha nchi tajiri kati yake na kupinganisha nchi za kaskazini na zile za kusini, bila kusahau nafasi ya kundi la « Cairns » (nchi 15 ambazo hazitoi msaada kwa usafirishaji nje wa bidhaa za kilimo).
Hapa Doha, kundi mpya
limeumbika. Kundi hili
lajulikana kama « Friends of the Development Box ». Kwa niaba ya
kundi hili, Muungano wa Ulaya, Marekani na kundi la « Cairns »
husahau wakulima maskini wa nchi zinazoendelea. « Friends of the
Development Box » latetea kwamba « sanduku la maendeleo »
ndilo msingi wa maafikiano juu ya kilimo. Sanduku hili lingesababisha kuwezekana
kwa utekerezaji wa mipango dhahiri ya kuendeleza kazi ya wakulima. Vile vile
sanduku hili lingetatua matatizo ya ukosefu wa chakula na kusaidia maendeleo ya
vijiji.(miongoni mwa kundi hili kuna nchi 14). Vyama vya mrengo wa kushoto vya
kifaransa vyapinda hii "Development box" (!!!).
Swala
la msaada wa serikali kwa ajili ya uzalishaji na usafirishaji wa bidhaa nje ya
nchi wazungumziwa pia (biliardi 380 za dola ya Marekani katika nchi za Shirika
la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD).
lajadiliwa pia swala la kufungua masoko ya nchi za Ulaya, ya Uswisi, Japan na
Korea.
Marekani
imeishaonyesha upinzani wake baadhi ya Development box. Muungano wa Ulaya, kwa
upande wake, umetangaza kuwa mswada wa taarifa unaomba mengi juu ya upunguzaji
wa msaada kwa usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi.
Inawezekana
kwamba kundi la Cairns litaunga mkono "Development box", ikiwa mbinu
maalum zinafasiriwa wazi (chakula, mipango ya kijamii). Wengi kati ya wajumbe wa
nchi tajiri wanasema kwamba mswada wa taarifa u jumla moja. Kuchunguza peke yake
sehemu moja ya jumla hii kungebomoa jumla yenyewe. Sasa wajumbe hawa
wanashawishi wenzao kukubali mswada kama ulivyo.
UTEKELEZAJI
; Mrahisishaji : waziri wa uchumi wa Uswisi
Utathmini
wa utekelezaji wa maafikiano yaliopo umekuwa kama uti wa mgongo wa umoja wa nchi
zinazoendelea kabla, mnamo na baada ya mkutano wa Seattle. Ni utathmini huu
uliosababisha kudumu kwa upinzani kati ya nchi za Kaskazini na nchi za Kusini,
ndani ya Shirika la Biashara Ulimwenguni, hasa hasa katika miaka ya hapa nyuma.
Vishawishi vilivyotumiwa kwa nguvu na Wanaulaya pamoja na Wamerikani kuhusu
jambo hili ndivyo vilivyouelegeza upinzani wa nchi zinazoendelea. Leo nchi hizi
hazisemi lugha moja juu hasa hasa ya swala la misaada.
Kinyume,
jambo la matumizi ya masoko ya vitambaa laendelea kutenganisha nchi
zinazoendelea na nchi tajiri. Kwa niaba ya nchi nyingi, jinsi swala hili
litakavyotatuliwa kutaathiri matunda ya mapatano mengine
NYANJA
MPYA (mambo ya Singapore ; mrahisishaji : waziri wa biashara ya kimataifa wa
Canada
Ni
mambo yaliyazushwa huko Singapore, katika mkutano wa kwanza wa mawaziri, na
yaliyopaswa kujadiliwa na makundi ya kikazi. : utegajiuchumi, sera ya mchuano,
masoko ya umma na urahisishaji wa biashara).
Hiki
ndicho kiini cha kutaka duru mpya kwa Muungano wa Ulaya, Marekani na marafiki
zao. Zinapopinga duru mpya, nchi zinazoendelea zina maoni mamoja juu ya jambo
hili, na umoja huu unadumu. Nchi zinazoendelea, hasa hasa nchi maskini
zinaendelea kuwa na upinzani imara. Bali kuna nchi za Marekani ya Kusini
zinazoonyesha vivuli.
MAZINGIRA
; mrahisishaji : maibu waziri wa mambo ya nje wa Chile
Muungano
wa Ulaya una msimamo mkari kuhusu mazingira. Waomba kuwepo kwa kanuni ya
uangalifu, mwafaka kati ya maafikiano ya Shirika la Biashara Ulimwenguni na
maafikiano ya kimataifa juu ya mazingira pamoja na maafikiano juu ya lebo.
Muungano
wa Ulaya unakubali kwamba mapatano hayangelianza kabla ya mkutano wa 5 wa
mawaziri ambao unatarajika kuwepo katika mwaka wa 2003. Maoni haya yanaungwa
mkono na nchi za Norway, Japan na Uswisi. Walakini jinsi zinavyochunguzwa feli
zinazozingatia mapendekezo ya nchi zinazoendelea hupunguza hali ya kuaminika ya
Wanaulaya, hasa wanapothibitisha hawana nia ya kufuata sera ya kulinda viwanda
vya nchini.. Ingawa kuna watu wanaosema kwamba kuacha kwa Muungano wa Ulaya kwa
mahitaji yake juu ya nyanja mpya kungeeleweka kama ufunguo unaopewa nchi
zinazoendelea kwa ajili ya mazingira, Muungano wa Ulaya unaonekana kuwa katika
hali ya upweke.
UUNDAJI
WA KANUNI ; mrahisishaji : waziri wa biashara na viwanda wa Afrika ya Kusini
Ulikuwa
ni mjadala juu ya kanuni zihusuzo misaada na kutokuwepo kwa ujazaji wa bidhaa
rahisi katika soko. Washawishi wa kimarekani hawataki mabadiliko yoyote yale,
wakati nchi zinazoendelea zataka uundaji utilie mkazo kwenye uchunguzi maalum na
ambao ni mmoja kwa wote.
Walipojadili
juu ya msaada unaopewa uvuvi, Marekani na Ufilipino zilipinga Muungano wa Ulaya.
Marekani yataka msaada huu upunguzwe.
Mrahisishaji
: waziri wa Fedha wa Mexico
Mswada
wa taarifa tofauti juu ya haki za kitaaluma ulichunguzwa bila kuhusisha mambo na
yaliyojadiliwa huko Seattle. Nguvu nyingi zachukuliwa na swala la madawa. Nchi
ya Bolivia ndiyo peke yake iliyosema kitu juu matumizi ya hati. Katika siku hizi
mbili zilizopita, mjadala ulifanyika juu ya aya ya nne ya mswada wa taarifa. Aya
hii ingelegeza kidogo misimamo mbali mbali.maandiko ya msingi.
Aya
yenyewe, sasa ambapo naandika, inakuwa kama ifuatavyo "We agree that
the TRIPS Agreement does not and should not [ou : shall not] prevent Members
from taking measures to protect public health. Accordingly, while reiterating
our commitment to the TRIPS Agreement, we affirm that the Agreement can and
should [ou: shall] be interpreted and implemented in a manner supportive of WTO
Members'right to protect public health and, in particular, to ensure access to
medicines for all. In this connection, we reaffirm the right of WTO Members to
use, to the full, the provisions in the TRIPS Agreement, which provide
flexibility for this purpose."
Aya
hii ilibuniwa baada ya mkutano wa mrahisishaji, Marekani, Muungano wa Ulaya,
Kenya, Nigeria, Brazil, India, Canada, New Zealand na Zimbabwe. Sasa wanajiuliza
kama inafaa kutumia maneno "can and should" ama "shall' ambalo
peke yake lina maadili ya kisheria.
Marekani
yapinga matumizi ya neno “shall”. Huenda siku ya leo tatizo hili
likatatuliwa ama likaahirisha mwishoni mwa mapatano haya.
Makubaliano
yanakwenda kama hivi : Maandiko yaliopa hayatagusiwa, wala juu ya madawa, wala
juu ya rasilimali ya ainasafu, wala juu ya mbegu, wala juu ya ujuzi wa mapokeo.
Hali kadhalika, kuhusu madawa, halijapewa suluhisho swala la madawa kutoka nchi
mbali mbali yanayoingizwa katika nchi zisizo na viwanda vya madawa. Nafasi kubwa
ilichukuliwa na maoni ya Wanaulaya. Ikumbukwe kwamba hapa Doha washawishi wa
wenye viwanda vya madawa wanatumia nguvu zote ziwezekanazo. Kwa niaba ya watu
hawa, wakiungwa mkono na Uswisi, hata aya inayohusika ambayo nimeishaitaja
inavuka mipaka inayokubaliwa.
Maafikiano ya mwisho yakitumia maneno « can and should », taarifa haitakuwa na maana yoyote ile ya kisheria.
Maswala mengine yalizushwa na baadhi ya wajumbe : ADPIC na viumbe anuwai, kuidhinishwa kwa maafikiano ya Cotonou pamoja na kanuni za kijamii (Muungano wa Ulaya), uangavu wa kanuni za kitaifa kuhusuana na kanuni za Shirika la Biashara Ulimwenguni (Muungano wa Ulaya, Marekani na Canada), mwenendo wa mambo katika tawi la Shirika la Biashara Ulimwenguni linalosuluhu migogoro (Japan), uhusiano baina ya ufanyajibiasharausimamizi wa fedha na madeni (Malaysia, Malawi, Pakistan na nchi nyingine zinazoendelea), viwango vya ushuru wa forodha viwandani (nchi maskini). Maswala haya hayakufanyiwa uamuzi.
Kutoka Doha
Raoul Marc Jennar
12 novemba 2001
Dr Raoul Marc JENNAR
Mtafiti kwenye Shirika Oxfam Solidarité (Brussels) na URFIG (Brussels-Paris-Geneva)
Site Web : www.urfig.org