Nyaraka
zinazotetewa na URFIG
OMC -
Shirika la Biashara
Ulimwenguni - WTO
Taarifa
la Geneva (6 juini 2001)
DUNIA
YETU SI YA KUUZWA
Shirika
la Biashara Ulimwenguni : Lipunguze nguvu ama lifutwe
Umewasili muda wa kusimamisha utandalizi na
kupigania shughli nyingine ambazo tuna uhakika uhakika zitasaidia kwa kujenga
dunia mpya. Kutoka na masauti mengi yasiyo na kifani ya wananchi na serikali
tofauti yaliyolipinga, Shirika la Biashara Ulimwenguni lilipoteza nguvu sana.
Mkutano wake wa tatu wa mawaziri uliofanyika mjini Seattle (USA) mnamo mwezi
novemba 1999, ulimomonyoa uhalali wa shirika hili. Tangu wakati huu, mamilioni
ya watu kukoka kwenye nchi maskini au nchi tajiri yamejiunga pamoja na kupiga
vita utandalizi kwa ajili ya kujenga hali mpya ya uchumi ambao i haki na ya
kutetea.
Baada ya mkutano wa Seattle, kutokana na kule kupinga uhalali wa shirika
la Biashara Ulimwenguni, kulitolea ahadi ya kurekebisha mambo. Walakini, hadi
leo, hakuna lolote lile lililofanyika. Bali mambo yaliharibika zaidi. Muda
umewasili wa kushusha nguvu na athari za Shirika la Biashara Ulimwenguni.
Ukosefu wa demokrasia, ukosefu wa uangavu na wajibu wa shirika hili ambalo
lingelipaswa kuendeleza biashara hulu, licha ya wajibu huu, umesaidia
kutajirisha wachache, kupaanisha shimo baina ya nchi tajiri na nchi maskini,
kufanya maskini jamii za wengi duniani, kuhamisha wakulima na wafanyakazi hasa
hasa katika nchi za ulimwengu wa tatu na kuhimiza njia za uzalishaji na za
kutumia uchumi zisizodumu.
Yametupiliwa mbale kinyama malalamiko ya wafanyakazi na wakulima,
malalamiko ya wateteyaji haki za binadamu na mazingira, ya viongozi wa kidini na
za wazalendo wa nchi tofauti, malalamiko ya Serikali za Ulimwengu wa tatu
yanayopinga kutokuwa na ulingano na kuzusha matatizo kunakotokana na na
utimilishaji wa duru ya Uruguay.Ofisi ya shughli za utawala wa Shirika la
Biashara Ulimwenguni inayojidai kutopendelea upande wowote ule, pamoja na kundi
la mataifa tajiri, vile vile na wateteaji wengine wa sera zake, kama kawaida,
wanatumia nguvu zao zote zile ili Shirika la Biashara Ulimwenguni linufaishe
wana biashara. Mbinu wanayoyitumia ni kusisitiza hali ya kuwa na mtazamo
usiojifunga ya Utandalizi. Mapatano yaliyotegemewa kujadili upya maafikiano juu
ya ulimaji, huduma, haki za wote kwa kuzalisha mali na biashara yamegeuzwa
mwendo. Wana utandalizi hupendelea hasa urekebishaji wa kasoro, jambo ambalo
linaharibu zaidi.
Serikali hudanganywa, ujanja watumiwa ili ukubaliwe mkutano wa nne wa
mawazili utakaofanyika nchini Katar tangu tarehe 9 hadi tarehe 13 novemba
mwakani. Mapatano mapya ya kupanulia zaidi njia Shirika la Biashara Ulimwenguni
yaandaliwa.Maparano haya yamepewa jina la utani la "duru ya
maendeleo". Jina hili ni la kuvutia tu. Lengo la kweli la duru hili ni
kupanulia wachache, kwa kupitia kwenye shirika la Biashara Ulimwenguni, haki za
kuzalisha mali, za kunufaika na masoko ya raia, na sera za mchuano nk.
Msaada wa namna hii unaopewa mapampuni ya kimataifa utadhoofisha zaidi
uchumi wa mataifa na majimbo, wa wafanyakazi, wakulima, wazalendo, manawake na
makundi mengine ya jamii. Msaada huu u hatari kwa afya na usalama, mazingira,
usalama wa wanyama porini. Matokeo yote haya husababishwa na ukosefu duniani wa
msimamo thabiti, mmomonyoko wa uchuni wa kitaifa, shimo kila siku kubwa zaidi
kati ya umaskini na utajiri ndani ya kila nchi hata baina ya nchi tofauti.
Shanzo cha maafa haya ni utandalizi usio na mipaka.
Umewasili muda wa kugundua hali ya hatari iwepo sasa biashara ya
kimataifa na shirika lake kuu ambalo ni Shirika la Biashara Ulimwenguni. Sasa
hivi, mwanzoni mwa karne la 21, hatuna budi kubadili mashirika ya kijadi, ambayo
ni si ya haki, bali ni ya kukandamiza. Twapaswa kubuni muundo mpya wa
kubadilishana, usiosahau haki za kijamii na ambao ni wa kudumu.
Twaita
ulimwengu ili bila kukawia :
-
Zilindwe tamaduni za aina mbali mbali, udumu utofauti wa kibiolojia, wa kijamii
na wa kiuchumi
-
Kuthibitisha hatua kwa hatua sera zinazotilia mkazo biashara na mabadilishano ya
kijimbo ; kudhamini haki za kiuchumi, za kijamii na za kitamaduni
zinavyojulikana kwa wote.
-
Kukarabati uhuru wa jamii tofauti na kudhibiti demokrasia kwa kiwango cha taifa
na jimbo.
Ili mambo haya yatekelezwe, sheria mpya zapaswa kutumika. Sheria hizi
zingezingatia udhibitishaji wa demokratia, ulinzi wa mazingira, uadilifu,
ushirikiano na tahadhari.
Kutokana na mambo haya,
twaomba serikali zetu :
Kutopaanisha Shirika la
Biashara Ulimwenguni
Twaeleza upya upindani wetu kwa kuanzisha upya duru nyingine ya mapatano,
upinzani wa kueneza wajibu wa Shirika la Biashara Ulimwenguni kwenye nyanja za
uzalishaji mali, sera za mchuano, masoko ya raia, bioteknolojia na uhuru wa
viwango vya ushuru wa forodha.
Kuenea kazi ya Shirika la Biashara Ulimwenguni kwenye nyanja za
uzalishaji mali na sera za mchuano, ama kuarmisha mataifa yote kufuata muundo wa
Shirika la Biashara Ulimwenguni kuhusu masoko ya raia (mwanzoni uangavu ukiwa ni
lazma), kungelikuwa kinyume na uhuru wa kila nchi. Vile vile kungeliweka katika hali ya hatari makampuni madogo
na ya kati kati. Kungelishusha maendeleo ya ulimaji na uchumi majimboni.
Kungeliathari vibaya jamii na mazingira.
Hatutaki mbinu mpya zitumiwazo na Muungano wa Ulaya za kuunga mkono
mapatano mapya juu ya uzalishaji mali na muchuano katika maafikiano ya
kimataifa. Inafaa kwa sasa Shirika la Biashara Ulimwenguni likatazwe kueneza
uhuru wa biashara. Badala yake, inafaa lipatikane bila kungoja suluhisho kwa
maswala ya dhuluma yanayokumbana nao mataifa ya ulimwengu wa tatu. Hayana
uhusiano wowote ule na mapatano juu ya kueneza uhuru wa biashara.
Shirika la Biashara Ulimwenguni li mbali na
wajibu wake : Kulinda haki na mahitaji muhimu na kijamii
Kwa
nini haki za kijamii na mahitaji muhimu yachunguzwe kwanza na Shirika la
Biashara Ulimwenguni ? Jibu hatuna. Maafikiano ya Shirika la Biashara
Ulimwenguni hayangelihusu mahitaji ya kijamii au ulinzi wa dunia : chakula,
maji, huduma muhimu jamiini, elimu, afya, usalama wa watu, mazingira na ulinzi
wa viumbe hai. Kutwaa bila halali kwa sheria za kibiashara katika nyanja hizi
kumeishazusha upinzani wa raia dhidi ya viumbe vilivyobadilika kwa vinasaba,
dhidi ya uharibifu wa mapori ya asili, dhidi ya upelekaji katika nchi za nje wa
vitu vyenye sumu ambavyo vimeishafukuzwa katika nchi vitokamo, dhidi vile vile
ya utangazaji wa sifa za tumbaku unaofanywa kinyama na makampuni yake.
VIPI
NA MAAFIKIANO MAKUU KUHUSU BIASHARA YA HUDUMA (GATS) ?
WALINDWE
RAIA, ZILINDWE HODUMA ZA KIJAMII
Nyanja kama vile afya,
elimu, nguvu za umeme na mahitaji muhimu zisilazimishwe kutii kanuni za biashara
ya kimataifa. Katika Maafikiano Makuu Kuhusu Biashara ya Huduma (GATS) na
katika nyaraka nyingine kumeandikwa kwamba usambazaji wa uhuru wa biashara na
uzalishaji mali ngambo vina athari mbaya sana, kwa mfano, kwenye huduma muhimu.
HATUTAKI
HATI ZA KUDHAMINI SOKO KWA MAKAMPUNI MACHACHE :
MBEGU
NA MADAWA ZI MAHITAJI MUHIMU YA BINADAMU, SI
BIDHAA
Sera zote zihusuzo
rasilmali ya kitaaluma zingeliruhusu serikali mbalimbali kutotoa hati zinazoenda
kinyume na ulinzi wa afya na usalama. Hati ambazo zingelihusika hasa hasa ni
zile zinazohusu madawa na afya. Hati zinazohusu viumbe hai, ikiwa ni vidudu
lazma zikatazwe na sheria zote za kitaifa au za kimataifa.
Sheria za leo juu ya rasilimali za kitaaluma
zinavyoandikwa katika maafikiano ya kibiashara, kama vile maafikiano juu ya
matawi wa rasilimali ya kitaaluma yahusuyo biashara huzuia watu kupata madawa na
vitu vingine muhimu. Vile vile huweka mikononi mwa wachache maisha ya viumbe na
ujuzi wa zamani, huzuia uhuru wa viumbe anuwai na huwa kipingamizi kwa maendeleo
ya kijamii katika nchi maskini kuliko nyingine.
Hakuna haja ya kuingiza haki za rasilimali ya
kitaaluma katika maafikiano ya kibiashara.
KUSIWEPO
HATI JUU YA VIUMBE HAI
Sheria
za kitaifa na za kimataifa hazina budi kukataza hati zihusuzo viumbe hai na
rasilimali ya kitaaluma za aina hii.Utofauti wa vinasaba si mali binafsi ya
wamoja. Hivyo, umiliki wa maisha pamoja na wa ujuzi wa kitamaduni ni uharamia.
Sharti usimamishwe.
KILA BINADAMU ANA HAKI KWA CHAKULA :
USIMAMISHWE UDANGANYIFU JUU YA MAAFIKIANO JUU YA ULIMAJI
Maafikiano
juu ya ulimaji hudanganya watu. Msaada kwa ulimaji wa kiwiwanda, ambao
umeelekezwa kwenye biashara ya nje, haukupunguzika kamwe. (Bali umeongezwa),
ingawa kazi na maisha ya wakulima wadogo wadoko hudhoofishwa na uhuru wa
kuingiza bidhaa.
Ili
wakulima hawa wasisahaulike, hatuna budi kupunguza sana msaada kwa biashara ya
nje ya mazao ya kilimo, na kutazama upya uhuru katika uingizaji wa bidhaa.
Hatua
za kulinda walimaji wadogo wadogo zisirudishwe nyuma na sheria za biashara ya
kimataifa.Muundo wa kibiashara usiharibishe kiwango cha maisha ya wakulimu
wadogo, wavuvi na raia wananchi.
Haki
za kila mtu kwa chakula haziwezi kuwepo ikiwa uhuru kwa chakuli haudhaminiwi,
yaani haki ya kila jamii kwa kujichagulia sera pekee kuhusu chakula na kilimo,
pamoja na haki kujitaftia chakula kufuatana na mila na tamaduni zake.
KUSIWEPO HURIA KATIKA KUTEGA UCHUMI.
Maafikiyano
ya Shirika la Biashara Ulimwenguni juu ya vitegauchumi vinavyohusu biashara
hayana budi kubadilishwa. Mataifa yote, hasa hasa yale maskini, hupaswa
kujichagulia sera ambazo zinahimiza uzalishaji mali wa kizalendo na kuendeleza
viwanda vidogo vidogo vya kitaifa kwa ajili ya maendeleo. Kubadilishwa kwa
maafikiano haya kusiunge mkono wajibu wa Shirika la Biashara Ulimwenguni katika
uwanja wa kutega uchumi. Ndiyo maana twapinga na kukata katakata maafikiano
mapya ndani ya Shirika la Biashara Ulimwenguni juu ya sheria za vitegauchumi,
juu ya muundo wa kutega uchumi au juu ya utegeji uchumi wowote ule.
Mapendekezo
kama yale ya Maafikiano Makuu Kuhusu
Biashara ya Huduma (GATS) ama yale yanayodai kutumia uangavu katika uwanja wa
kutega uchumi, au yale juu ya maafikiano yanayojumuisha nchi nyingi ni mbinu tu
za kiujanja zenye lengo la kushawishi mataifa au mashirika yaliyokata kuunga
mkono maafikiano ya kiujumla juu ya vitegauchumi. Shabaha lenyewe ni kunufaaisha
wategani uchumi kutoka ugenini. Twatupilia mbali mbinu zote hizi ambazo hasha
hazitofautiani na MAI.
KWA
AJILI YA USAWA KATIKA UFANYAJI BIASHARA :
TOFAUTI
NA UPEKEE KATIKA VITENDO
Kaika biashara ya
kimataifa, inafaa uzingatiwe umaskini wa mataifa ya ulimwengu wa tatu. Bila haki
hii, nchi maskini kamwe hazitafaidika kwa biashara ya kimataifa.
KWANZA
HAKI ZA KIJAMII NA MAZINGIRA
Huria ya biashara
hupendelea faida ya makampuni kuliko ile ya raia na mazingira. Tuna haja ya
biashara inayofanyika kwa kutovunja haki za watu. Vile vile, inafaa ziheshimike
haki za binadamu pamoja na haki za wafanyakazi, bila kusahau zile zinazohusu
mazingira, afya, elimu, haki za wazalendo, haki za kimaendeleo, zile zinazohusu
usalama wa watu, usalama wa chakula na usalama wa wanyama wa porini.
Kwa mfano, azimio la
Shirika la Kazi Duniani (ILO) juu ya haki za kimsingi kazini, Maakala juu ya
viumbe anuwai, itifaki juu ya usalama wa kibiolojia pamoja na azimio la Umoja wa
Mataifa juu ya haki za binadamu hupaswa kufanikishwa ifaavyo.
Ili zifanikishwe haki
wafanyakazi na haki nyingine za binadamu, hatunabudi kushawishi mashirika ya
kimataifa yanayohusika.
TWAAKA
KUWE NA DEMOKRASIA KATIKA KUFANYA UAMUZI
Jamii zina haki ya
kujichagulia mfuno wa kimaendeleo na zina haki ya kujulishwa yanayofanyika
katika uwanja wa biashara ya kimataifa. Jamii hizi zaomba kujulishwa jinsi
uamuzi unavyofanya katika maafikiano. Jamii hizi zataka pia kuwe uangavu,
demakrasia na mfungamano katika shughli za mashirika ya kimataifa. Shughli za
Shirika la Biashara Ulimwenguni zaendeshwa kisiri na hazishirikishi nchi nyingi
na kusahau wataalamu wasiotegemea serikali. Shirika la Biashara Ulimwenguni
limewekwa mikononi mwa serikali chache, ambazo vile vile kwa upande wake zi
mikononi mwa makampuni beberu ya kimataifa.
KUPINGA
MUUNDO MWENYEWE
Tawi la Shirika la Biashara Ulimwenguni la
kutatua migogoro la kukubaliwa : latumia muundo ambao si halali wa sheria
zisizona haki. Kadhalika, muundo huu wakosa demokrasia. Pia hujichukulia kwa
nguvu wajibu wa kutunga na kutiisha sheria, wajibu ambao kwa kawaida u wa nchi
huru au majimbo totauti.
Ili muundo wa biashara ya kimataifa uwe halali,
inafaa pia kuwe na mabadiliko ya maana nje ya Shirika la Biashara Ulimwenguni.
Muundo kama huu hauna budi kuzingatia kwanza haki na ubora wa maisha vya
wafanyakazi na wakulima ambao huzalisha bidhaa na huduma. Hakuna serikali ama
shirika la kimataifa ambalo lingeliruhusiwa kujisahaulisha jinsi mashirika ya
kimataifa na serikali furani zinavyoshambulia haki za kimsingi za wafanyakazi na
zinavyodharau haki zilizoishatambuliwa na wafanyapazi, bila kusahau upotovu wa
usalama wa kazi na jinsi mishahara inavyopunguzwa. Lazima, popote pale
ulimwenguni, haki za wafanyakazi zikazwe.
Vile vile, sharti Shirika la Kimataifa la
Fedha, Benki ya Dunia na benki nyingine za kimaendeleo zifute 100% madeni ya
nchi maskini, ili nchi hizi zipambane na umaskini mwenyewe. Ratiba za
kurekebisha kimuundo hali ya uchumi zenye lengo la kuleta huria zinapaswa
kusimamishwa. Inafaa, katika Umoja wa Mataifa, serikali zijadili kidemokrasia
ili kuwe maafikiano yanayolazimisha makampuni ya kimataifa hutovunja haki za
binadamu, mazingira na demokrasia.
Sisi,
tunao piga sahihi kwenye taarifa hili, tumejituma kutumia nguvu zetu zote ili
biashara ya kimataifa ifanyike ifaavyo, iwe halali kijamii na ichungwe
kidemokrasia. Twaia serikali zetu ili zitafute masuluhisho bora kwa maswala
tuliyoyataja hapa juu na kupungua ubeberu wa Shirika la Biashara Ulimwenguni.
Lazima Serikali hizi zirekebishe kinaganaga uundo wa Shirika hili. Twajituma
kuija raia wa nchi zetu ili wajiunge nasi ili maswali yetu yajibike na ipangue
sera bovu ya Shirika la Biashara Ulimwenguni.Tutaunga mkono watu wengine ambao
kama sisi, huendesha kampeni za kutetea umoja wa kimataifa. Twajituma kueneza
popote pale duniani ari ya Seattle na kuzuia Shirika la Biashara Ulimwenguni
kuanzisha wa duru mpya ya mapatano ambao inatarajika huko Katar.
(Maarifa
yaliyopigiwa sahihi na mamia ya mashirika kutoka pembe zote za dunia,
Déclaration de Genève - Notre monde n'est pas à vendre - OMC : la soumettre ou la supprimer (6 juin 2001)