Nyaraka
zinazotetewa na URFIG
OMC -
Shirika la Biashara
Ulimwenguni - WTO
MSWADAJARIJIO
WA KASHFA WA TAARIFA MAALUM YA MKUTANO WA MAWAZIRI WA SHIRIKA LA BIASHARA
ULIMWENGUNI
(Oktoba
30, 2001)
Mswadajaribio ambao hivi
karibuni uliandikwa kwa ajili ya mawaziri wa Shirika la Biashara Ulimwenguni
waja kama maafa kwa nchi maskini na kwa nchi zinazoendelea. Vile vile
mswadajaribio huu wapuuza mapendekezo ya shirika la raia wa ulimwengu
Shirika la Biashara
Ulimwenguni halina demokrasia yoyote ile. Mswada wapitishwa kwa nguvu ili
ujadiliwe katika mapatano yanayotarajika, ingawa wapingwa na wanachama wengi wa
Shirika la Biashara Ulimwenguni pamoja na waakilishi wa raia.
Leo, makundi ya
waakilishi wa raia kutoka kwenye pembe zote za dunia wametupilia mbali
mswadajaribio wa taarifa ya mawaziri watakaokutania jijini Doha kwenye mkutano
wa Shirika la Biashara Ulumwenguni. Msadajaribio wa nyaraka ya kutumiwa kwenye
mkutano wa Shirika la Biashara Ulimwenguni unaotarajika tangu tarehe 9 hadi
tarehe 13 Doha, nchini Katar, haukukubaliwa na wawakilishi wa raia.
Hali kadhalika, nchi
maskini ambazo zahisi dharau hazina imani kwenye mswada huu huu ambao waandikwa
kama vile wanachama wote wameisha kubaliana juu ya ajenda mpya ya Shirika la
Biashara Ulimwenguni, jambo ambalo si la kweli.
MaNGO’s kutoka kwenye
pembe zote za dunia yaomba mataifa tofauti yatokamo kupinga nyaraka hii ambayo
si halali. Mashirika haya yataka mataifa yazuie mswada huu kutumiwa katika
mkutano wa Doha wa mawaziri wa Shirika la Biashara Ulimwenguni.
Nyaraka hii imeandikwa
baada ya mswaada mwingine ambao ulitupiliwa mbali na wajumbe wa nchi maskini
ambazo ni wanachama wa Shirika la Biashara Ulimwenguni. Nyaraka mpya, kama ile
ya kwanza, haizingatii mapendekezo muhimu ya nchi zinazoendelea, bali huingiza
mambo mengi yaliyopingwa na nchi hizi ambazo ni wanachama wa Shirika la Biashara
Ulimwenguni.
Mashauriano ambayo mwezi
jana yalifanyika kwenye Shirika la Biashara Ulimwenguni yalisababisha nyufa
zaidi, yalipopendekeza mswada ambao kaurekebishi kamwe nyaraka inayopingwa na
wengi.
Hali hii ya mambo
yapaanisha ufa katika ukosefu wa demokrasia ndani ya mfumo wa Shirika la
Biashara Ulimwenguni. Miezi mingi imepita wengi kati ya wanachama binafsi wa
Shirika la Biashara Ulimwenguni wakikataliwa kupitisha mapendekezo yao.
Kinyume na yanaoandikwa
katika nyaraka, nchi wanachama wa Shirika la Biashara Ulimwenguni hazikubaliani
juu ya ajenda ijao ya shirika hili. Hata tangu kabla ya mkutano wa Seattle wa
mawaziri wa Shirika la Biashara Ulimwenguni, nyingi kati ya nchi zinazoendelea
zimeomba kushughlikiwa kwa dosari na ukosefu wa haki ndani ya Shirika la
Biashara Ulimwenguni.. Walakini Marekani imekuwa kipingamizi.
Muungano wa Ulaya, kwa
upande wake, unatetea kuziidishwa kwa nyanja zinazoshughlikiwa na Shirika la
Biashara Ulimwenguni, kama vile utegaji uchumi, sera ya mchuano, jambo ambalo
halikukubaliwa na nchi zinazoendelea
Upinzani mkubwa
waonekana pia juu ya mambo kuhusu ulimaji. Kwa niaba ya nchi zinazoendelea,
lazma mkazo utiliwe kwenye kutosha kwa chakula na maendeleo ya vijiji. Marekani
na Muungano wa Ulaya hupendekeza zaidi kulindwa kwa masoko yake, kukiwapo
misaada na mikopo ya mahuruji.
Ingawa mengi kati ya
mataifa wanachama wa Shirika la Biashara Ulimwenguni yataka majadiliano mapya
juu ya sera za kukataza ujazaji wa bidhaa rahisi katika soko, Marekani haitaki
kusikia pendezo hili. Hali tofauti, katika mswada mpya, nyanja kama vile utegaji
uchumi, na sera za mchuano zilipewa nafasi kubwa kwa ajili ya mapatano yajayo.
Kinyume, katika mswada
mpya, orodha ya mapendekezo ya nchi wanachama wa Shirika la Biashara Ulimwenguni
ambazo si tajiri imefutwa. Katika mapendekezo haya, nchi zinazoendelea zatangaza
mambo ya kuchunguza upya ama ya kurekebisha kabla ya majadiliano mapya ndani ya
Shirika la Biashara Ulimwenguni.
Kutokana na maafikiano
yanayotumiwa sasa katika Shirika la Biashara Ulimwenguni, hisa ya nchi maskini
kuliko nyingine katika biashara ya kimataifa ilipunguka. Hali kadhalika, sera za
nchi hizi kuhusu nyanja kama maendeleo na afya zimeshambuliwa, eti zavunja
sheria ya Shirika la Biashara Ulimwenguni.
Mswadajaribio mpya
wanuufaisha Marekani, ukisisitiza kwamba hakuna limoja kati ya mambo haya
litakalochunguliwa, ikiwa nchi zinazoendelea hazilegezi mapendekezo yake.
Mswadajaribio mpya
wadharau pia wawakilishi wa raia ya wakulima, wavuvi, wafanyakazi na wenye
kutetea hali safi ya mazingira, ambao, kutoka nchi tofauti, walijadiliana na
kufanya kazi ya pamoja tangu miaka mingi kabla ya mkutano wa kiwaziri wa
Seattle, hadi leo.
Makundi mengi ya
wawakilishi wa raia na ya wafanyakazi wamejiunga pamoja na kusema : “Dunia
Yetu Si ya Kuuzwa : kampeni ya kutekea kurekebishwa ama kufutwa kwa Shirika la
Biashara Ulimwenguni”. Kampeni hii yaita wanachama ili wafikiri juu ya kuwepo
kwa Shirika la Biashara Ulimwenguni halili.
Mapendelezo ya makundi
haya ambayo yanaundwa na mashirika kukoka kwenye nchi zinazoendelea na nchi
tajiri, mashirika ya wafanyakazi na ya wakulima vile vile yalipuuzwa katika
mswadaratibio mpya ulioandaliwa kwa ajili ya mkutano wa mawaziri.
Ukaidi wa Ofisi ya
Shirika la Biashara Ulimwenguni na wa nchi chache tajiri ambazo hushawishi
Shirika la Biashara Ulimwenguni kutozingatia mapendekezo ya nchi zinazoendelea
na ya wawakilishi wa raia utaufanya mkutano wa kiwaziri wa Doha uletee balaa
mengi kati ya mataifa yatakayo hudhuia mkutano huu, au utaufanya mkutano huu
ushindwe kama vile ulivyoshindwa mkutano wa Seattle: ukataji hapo hapo au
taarifa batili
Wenye kutia sahihi
kwenye taarifa
*Alliance for Democracy,
U.S.
Wasiliana na Ruth Caplan
(Washington DC): 202-244-0561
*Arab NGO Network for
Development, Lebanon
Wasiliana na Ziad Abdel
Samad (Beirut): +961-1-319-366
*ECOROPA, France
Wasiliana na Agnes
Bertrand (Sauve): 33-4-66-77-0704
*Focus on the Global
South, Thailand
Wasiliana na Aileen Kwa
(Geneva): 41-22-791-8050
*Friends of the Earth
– International
Wasiliana na Alexandra Wandel (Brussels)
+32-2-542-0185 au Ronnie Hall (London)
*Global Exchange, U.S.
Wasiliana na Juliette
Beck (San Francisco): 415-255-7296 x 254
*IBON Foundation,
Philippines
Wasiliana na Tony Tujan
(Manila): +632-714-1580
*Institute for
Agriculture and Trade Policy, U.S.
Wasiliana na Shefali
Sharma (Geneva) +41-22-789-0724 na Sophia Murphy
(Minneapolis)
+612-870-3454
*Institute for the
Re-localization of the Economy, France
Wasiliana na Agnes
Bertrand (Sauve): 33-4-66-77-0704
*Public Citizen, U.S.
Wasiliana na Margrete
Strand (Washington DC): +202-454-5106
*Via Campesina,
International
Wasiliana na Nico
Verhagen (Brussels): +32-2-343-8444
*URFIG (Unité de
Recherche, de Formation et d'Information sur la Globalisation - Ofisi ya
Utafiti, Ushauri na mMarifa juu ya Utandalizi)
Wasiliana
Raoul Marc Jennar (Brussels) : 32 478 913 812
THE
DESASTROUS LATEST DRAFT OF WTO MINISTERIAL DECLARATION