Nyaraka zinazotetewa na URFIG kuhusu :

OMC - Shirika la Biashara Ulimwenguni - WTO

 

 

Nchi Maskini zatangaza kutokuwa tayari

kwa duru mpya ya mapatano ya kibiashara

na Yash Tandon

Mwenyekiti

Habari juu ya Biashara katika Afrika ya Kusini na ya Mashariki na Uamuzi wa Mapatano

(Southern and Eastern African Trade Information and Negotiations Initiative-SEATINI)

(Makala iliyotangazwa kwenye  http://wtoaction.org/discuss)

 

Tangu tarehe 22 hadi tarehe 24 Julai 2001, mataifa 49 ambayo ni maskini kuziidi mengine yamekutania Zanzibar na kwa sauti moja yakatangaza kwamba hayatashiriki kwenye duru mpya ya mapatano ya kibiashara ambayo yatarajika kufanyika huko Doha.

Baada ya kushindwa kwa mkutano wa Shirika la Biashara Ulimwenguni uliofanyika mjini Seattle, mataifa tajiri, hasa hasa yale ya Muungano wa Ulaya, yajaribu kushawishi nchi maskini kuunga mkono duru mpya.

Huko Zanzibar, nchi maskini hizi, zote kwa pamoja, zilitangaza kuwa « …Kutokana na uhaba wa nguvu za nchi maskini, mapatano ya kibiashara ya kimataifa yatazingatia ukosefu huu wa nguvu ambao unasababisha kutoweza kwa nchi hizi kushiriki ifaavyo kwenye mapatano haya yenye ajenda pana. Vile vile nchi hizi hazitaweza kufuata masharti mapya» (Ratiba ya maendeleo ya nchi maskini kwa ajili ya mkutano wa 4 wa Mawaziri wa Shirika la Biashara Ulimwenguni. Mkutano huu ni wa kujadili juu ya malengo na mapendekezo – LDC/MM/ZNZ/3, 24 julai 2001).

Katika hotuba yake ya kufunga mkutano, Bwana Iddi Simba, Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania alifafanua hali ya mambo : « Kufuatana na jinsi tulivyoelewa, lengo la nchi tajiri ni kuanzisha huko Doha  duru mpya ya mapatano ya kimataifa na ya kibiashara. Nyingi miongoni mwa nchi maskini zingependa zaidi kurekebisha na kutekeleza maafikiano ya duru ya Uruguay na kuendeleza mapatano juu ya utathmini wa maafikiano haya na ajenda ya muundo wa Shirika la Biashara Ulimwenguni. Wengi kati yetu hatuwi tayari kwa duru mpya. Kwa niaba yetu, kuna sababu nyingi za kupinga duru mpya. »

Kwa mfano, nchi maskini zaogopa vikwazo ambavyo huenda vitafuata kutoweza kuheshimu masharti mapya ambamo nchi hizi zitakuwa zimejiingiza «Shirika la Biashra Ulimwenguni ni ofisi ya mapatano ambayo huzaa masharti na kubuni vikwazo kwa wale wasioyaheshimu masharti haya. Hatuna budi kuwa na makini kabla ya kutoa uamuzi juu ya masharti mapya. Hali kadhalika, twapaswa kukataa kuingizwa kwa nguvu ndani ya duru mpya ambayo wengi kati yetu hawawezi hata kufafanua. U mpana wajibu unaotokana na Muundo Wa Biashara ya Kimataifa ( Système Commercial Multilatéral -SCM). »

Katika maandiko ya mwisho ambamo kuna « Malengo na Mapendekezo ya Mapatano», wajumbe wa nchi maskini wamebadilishana mawazo juu ya maswala matato muhimu : soko kwa wote, utekelezaji wa maafikiano na ajenda. Huhusu soko, mkazo ulitiliwa kwenye Mashati ya Asili. Bangladesh, ikisaidiwa na Nepal pamoja na Bhutan, zimetaka Masharti haya yawe na « huria » ili kila nchi ijichagulie soko kwa njia halali.

Bali, wajumbe wengi walipinga neno « huria ». Baada ya mazungumzo ya muda mrefu, wajumbe wamekubaliana kubadili neno « huria » na kutumia « halisi na legevu. ». Vivyo wajumbe walikubaliana na umoja ukarudi ndani ya kundi la nchi maskini.

Walikubaliana pia kutumia popote maneno bora zaidi na kubadili neno « huria ». Rais amefasili kwamba, kwa niaba ya nyingi kati ya nchi maskini, hiria ilirudisha nyuma maendeleo ya viwanda na kuziidisha umaskini na ukosefu wa kazi. Neno «Hulia » limegeuka kama matusi katika msamiati wa nchi maskini au wa nchi zinazoendelea kwa ujumla.

Kuhusu utekelezaji wa maafikiano yaliopo, wajumbe wameandika maswala ambayo « wanatumaini kutatua kabla, mnamo na baada ya mkutano wa Doha ». Miongoni mwa maswala haya kuna mambo yanayopaswa kufanywa na nchi maskini katika uwanja wa kilimo, huduma misaada SPS na TBT, vitambaa vya nguo, maafikiano MIC, ADPIC, utathmini wa utathmini wa forodha, shughli za kupinga uzajazi wa bidhaa rahisi katika soko na fidia pamoja na hifadhi : « Nchi maskini ziepushwe na hifadhi yoyote ile. Nchi maskini ambazo zatumia hifadhi lazma zisifuate fidia. »

Kuhusu ajenda ambayo inatarajika kujadiliwa Doha, nchi maskini zimeonyesha msimamo wake juu ya ulimaji, biashara ya huduma pamoja na haki za asilimali ya kitaaluma. Baadhi ya kanuni zinazoandikwa katita haki hizi za kiataaluma zitarekebishwa upya katika mkutano wa Doha. Msimamo wa Nchi Maskini juu ya kanuni ya 27.3b ni huu ufuatao : urekebishaji wa kanuni hiyi utapaswa kutilia mkazo kwa « kutotoa hati yoyote ile » iliwa inahusika mimea, wanyama, sehemu za mimea na za wanyama, ikiwemo utafiti wa kivinasaba na kibiologia kwa ajili ya kupata mimea, wanyama, na sehemu zake. Sasa i wazi kuwa hati kuhusu viumbe hai zimetupiliwa mbali.  Wajumbe walitangaza pia kwamba : « utoaji wa hati juu ya madawa wa kimsingi kufuatana na orodha ya  Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughlika na Afya zapaswa kukatazwa».

Miongoni mwa wajumbe waliokutania Zanzibar kulikuwa Nchi Maskini nyingi ambazo ambazo si wanachama wa Shirika la Biashara Ulimwenguni. Nyingi kati ya nchi hizi ziliomba kuwa wanachama na bado hazijaingizwa ndani mwa Shirika hili. Tangu 1997, nchi maskini sana zimekubaliwa kuwa wanachama wa Shirika la Biashara Ulimwenguni. Sababu ni kuwa ugumu ughali na masharti mengine ya kukubaliwa kuwa mwanachama wa Shirika la Biashara Ulimwenguni. Huko  Zanzibar, Nchi Maskini zilipendekeza kuwa : « Kutokana na hali ya kipekee ya uchumi, ukosefu wa fedha, umaskini wa kibiashara na kutoendelea kwa Nchi Maskini, katika mapatano wa kuingizwa, wanachama wa Shirika la Biashara Ulimwenguni wangelipaswa kutoshurtisha mengi juu ya asilimali ama huduma zinazokuwa katika Nchi Maskini, kufuatana na na mapendekezo ya Mkutano wa Mawaziri yanayozitetea nchi hizi. »   

Nchi Maskini zapendekeza kwamba katika mapatano ya Doha mambo mawili yatiliwe mkazo zaidi. Jambo la kwanza ni kuwa hali ya kila nchi maskini ichunguzwe kipekee.  Jambo la pili linahusu msaada wa kitaalamu ambao utazisaidia nchi maskini kujadiliana na nchi nyingine ifaavyo katika mapatano ya kisasa na kuweza kushiriki katika muundo wa biashara ya kimataifa. 

Kinyume na yanayopendekezwa na nchi tajiri ili yajadiliwe huko Doha, Nchi Maskini hazi zilizokutania Zazimbar hazikutaja sana « nyanja mpya ». Miongoni mwa nyanja hizi mpya ambazo nchi tajiri zingelipenda sana zipewe nafasi kubwa kwenye ajenda ya Doha kuna zile zilizochaguwa katika mkutano wa Singapore, yaani biashara na utegajiuchumi, sera za mchuano, uangavu katika soko za kiraia, urahisi katika mabadilishano. Vile vile kuna zile zilizochaguliwa katika mkutano wa Geneva na nyanja nyingine kama vile kanuni za kazi, mazingira na bei iviwandani.

Nchi Maskini zilifafanua kutohusika kwake na nyanja hizi. Hali kadhalika, nchi hizi zilitangaza ukosefu wake wa uwezo «kivifaa, tiufundi na kisaikolojia », ili ziendeshe mapatano juu ya nyanja hizi (kama alivyosema rais).  Kwa niaba ya nchi maskini, maswala juu ya vitegaji uchumi, sera za mchuano na uangavu katira soko za kiraia zachunguzwa sasa katika makundi tofauti ya kikazi za Shirika la Biashara Ulimwenguni. Kazi za makunzi haya bado hazijamalizika, ndiyo maana hakuna haja sasa ya kuanzisha mapatano mapya juu ya nyanja hizi

Msimamo wa Nchi Maskini kuhusu « biashara na mazingira » ulikuwa wa kuunga mkono mapatano yanatoendeshwa sasa na Kamati ya Biashara na Maendeleo. Nchi hizi zatangaza kwamba mapatano haya ya muhima. Sharti yaendelezwe. Bali nchi maskini zilionya kwamba ulinzi wa kimazingira usitumiwe dhidi ya bidhaa kutoka kwenya nchi maskini». 

Biashara pekee yake si lengo. Ni kifaa ni kifaa cha kutoa kwenue umaskini na kuwekwa kando wale amabao ni maskini na wamewekwa kando katika jamii ya dunia. Nchi maskini na nchi tajiri zote zakubaliana kwa jambo hili. Katika bara la Afrika, nchi ambayo yasemekana imeendelea ni Afrika ya Kusini (wanaotaja nchi hii wajidanganya). Kabla ya mkutano wa Zanzibar, Afrika ya Kusini iliita nchi zote wanachama wa SADC katika mkutano wa Johannesburg. Lengo la mkutano huu lilikuwa ni kuhimiza nchi za SADC kukubali duru mpya la Doha. Kama nchi tajiri, Afrika ya Kusini inadai kwamba duru mpya itazisaidia nchi maskini. Bali, katika mkutano wa Zanzibar, Nchi Maskini, angalau zile ambazo zi wanachama wa SADC (ikiwamo Tanzania, Uganda, Zambia na Lesotho), zote kwa pamoja, zilikata katakata duru mpya la Doha.

Mara nyingi jamii tajiri zilijituma kukusaidia jamii maskini zaidi ulimwenguni. Huko Zanzibar zilisikika sauti za wale ambao ni maskini. Wajumbe walishangilia mkutano wa Nchi maskini huko Zanzibar. Mkutano huu ulithibitisha umoja wa mataifa 49 maskini zaidi ulimwenguni. Umoja huu unatafsiri vile vile maoni ya mataifa haya juu ya mkutano wa Doha. 

Swali linalobadi ni kujuwa kama huko Doha, nchi tajiri zitalisikia sauti hili la nchi maskini.

 

Zanzibar 24 julai 2001 

 

 

Les Pays les Moins Avancés (PMA) déclarent ne pas être prêts à prendre part à un nouveau cycle de négociations commerciales (Yash Tandon, 24 juillet 2001)